Na. Mwandishi wetu, Matukio Daima App.
KUELEKEA Kilele cha Pondeza Chumbuni Festival mwishoni mwa Wiki Hii, Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza amewasisitiza Wananchi kujitokeza kwa Wingi kwani kutakuwa na burudani kutoka kwa Wasanii mbalimbali sambamba na zawadi nono kwa Washindi na baadhi ya Washiriki.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kukamila Mchezo wa Mpira Miguu kati ya Shehia ya Mwembe Makumbi juu na Mwembe makumbi Bondeni katika kiwanja cha Chumbuni, Mbunge huyo amesema kuwa, katika Kilele cha Tamasha hilo kutatolewa zawadi mbalimbali ambazo hazijawahi kutolewa kokote kule.
"Mimi nataka kuwatoa wasi wasi wananchi na washiriki wa Tamasha hili kwa mwaka huu tutatoa zawadi nono ambazo hazijawahi kutolewa kokote, kikubwa wanannchi waendelee kujitokeza ili waje kushuhudia historia ambayo itaandikwa hapa Chumbuni," amesema.
Ameeleza kuwa zawadi kubwa ambayo itatolewa itakuwa ni fedha taslimu licha ya kiwango kuwa hakijawekwa wazi kwa sababu ya kuvutia tamasha hilo.
"Hatujaweka wazi kima cha Pesa ambacho tutakitoa ili kuepusha watu kuja kuumiza wakati sisi tumeweka Tamasha hili kudumisha Umoja wetu ndani ya Jimbo la Chumbuni," amesema Pondeza.
Aidha Amesema kuwa, ameridhishwa na na muitikio wa Watu mbalimbali kushuhudia Michezo inayoendelea katika Tamasha hilo.
"Mimi ninawashukuru sana, Wananchi kutoka Jimbo la Chumbuni n wengine kutoka katika Majimbo mengine kwa namna walivohamasika na kuja kushuhudia michezo inayoendelea katika Tamasha hili," ameeleza Pondeza.
Nao Viongozi wa Timu ya Mwembe Makumbi juu na Chini wamepongeza Mashindano hayo kuwa na hamasa huku wakimuomba mubunge huyo kuyafanya kila mwaka.
0 Comments