Na. Mwandishi wetu, Matukio Daima App.
CHAMA Cha Soka Mkoa wa Pwani (COREFA) kimepongezwa kwa kuanzisha kituo cha mpira kwa vijana wadogo Wilayani Kibaha.
Akizindua kituo hicho kaimu mkuu wa wilaya ya Kibaha ambaye pia ni katibu tawala (DAS) Moses Magogwa ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kuwa uwekezaji kwa vijana kutasaidia kuwa na timu bora za baadaye.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Pwani Robert Munisi alisema kuwa malengo ya kuanzisha kituo hicho na vingine kwenye kila wilaya itakuwa na vituo vitatu ambapo kutakuwa na vituo 21 kwa mkoa mzima ni kuibua vipaji na kuviendeleza.
Naye mratibu wa kituo hicho Abdulakarimu Alawi alisema kuwa jumla ya vijana 500 wa shule za msingi na sekondari ambapo vijana wanacheza kutegemeana na umri wao.
0 Comments