Header Ads Widget

TCDC YABAINI MAPUNGUFU KATIKA UTENDAJI KWA BAADHI YA VYAMA VYA USHIRIKA

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP DODOMA


TUME ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) imekuwa ikifanya ukaguzi wa mara kwa mara katika Vyama vya Ushirika lengo likiwa ni kubaini uzingatiwaji wa matakwa ya Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali inayohusiana  na utendaji wa Vyama vya Ushirika.


Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Mrajisi wa vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt Benson Ndiege Wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu utendaji kazi na Mpango was kuhimarisha Ushirika kwa Mwaka 2923/24.


Amesema katika kipindi cha mwaka 2022/2023  hadi kufikia Juni, 2023 TCDC ilifanya ukaguzi wa jumla ya Vyama vya Ushirika 4,712 kati ya vyama 7,300 vya ushirika kupitia  Ofisi ya Tume Makao Makuu na Ofisi za Warajis Wasaidizi wa Mikoa. 


"Matokeo ya kaguzi hizo  yalionesha kuwepo kwa mapungufu katika utendaji wa Vyama vya Ushirika hususan maeneo ya uandishi wa vitabu, urasimishaji wa mali za Vyama, utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu nyingine za Vyama, uzingatiaji wa miongozo ya Mrajis, na madeni ya muda mrefu katika taasisi za kifedha," Amesema.


Na kuongeza Kusema" Hatua zilizochukuliwa kwa Vyama vya Ushirika ni kuvunja Bodi 55 za Vyama vya Ushirika, kupeleka masuala 30 Polisi na masuala 47 yanashughulikiwa na TAKUKURU," Amesema Mrajisi.


 Aidha,  Amesema Tume imetoa mafunzo kwa watendaji 4,732 wa Vyama vya Ushirika kuhusu uandishi wa vitabu na viongozi wa vyama wametakiwa kujieleza.


Jitihada za kukabiliana na masuala yaliyobainika:


Amesema Jitihada zinazotekelezwa na Tume kwa kushirikiana na COASCO, Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) na wadau wengine ni pamoja na Mpango Maalum wa Mafunzo kwa Maafisa UshirikaHadi kufikia Juni, 2023 Maafisa Ushirika kutoka mikoa 16 ya Tanzania Bara walipatiwa mafunzo ya Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama.


Mikoa hiyo ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Njombe, Iringa, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Kagera, Mara, Kigoma, Simiyu na Geita, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.Mpango wa Mafunzo kwa Viongozi na Watendaji wa Vyama



HALI YA UPATIKANAJI NA USAMBAZAJI WA PEMBEJEO


Amesema hali ya upatikanaji na usambazaji wa pembejeo katika kuhakikisha kuwa wakulima na wanachama wa Vyama vya Ushirika wanahudumiwa kwa kusogezewa huduma karibu, Vyama vya ushirika vimekuwa vikiratibu upatikanaji pamoja na usambazaji wa pembejeo za kilimo.


"Hadi kufikia tarehe 30 Machi, 2023, jumla ya shilingi 449,922,623,196 (Shilingi 449.92 Bilioni) zilitumika kunununua pembejeo za kilimo kupitia Vyama vya Ushirika nchini kwa ajili ya wakulima kwa mazao mbalimbali," Amesema .


Amesema Mbolea iliyonunuliwa na kusambazwa kwa wakulima kupitia vyama vya ushirika ni Tani 1,266,435 yenye thamani ya  227,983,187,800 (Shillingi 227.98 Bilioni). 



HUDUMA ZA UGANI


Amesema upatikanaji wa huduma za ugani kupitia Vyama vya UshirikaTume ya Maendeleo ya Ushirika imeendelea kuhamasisha Vyama vya Ushirika kuhusu umuhimu wa upatinakaji wa huduma za ugani na pembejeo kwa wanachama kwa wakati. 


Hadi sasa, Vyama vikuu vya Ushirika vimeajiri maafisa ugani 175 ambao wameendeleea kutoa huduma za ugani kwa wakulima katika mazao ya Tumbaku, Korosho, Pamba na Kahawa. 


MWELEKEO WA TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA KATIKA KUIMARISHA USHIRIKA KWA MWAKA 2023/2024 


Amebainisha Tume ya Maendeleo ya Ushirika imelenga kwenye Kuimarisha Maendeleo ya Ushirika ambapo Tume ya Maendeleo ya Ushirika ambayo inahusisha Kamisheni, Menejimenti na Watumishi wengine, imejipanga katika mwaka 2023/2024 kutekeleza maeneo saba (7) ya Kimkakati yatakayolenga kufikia Kipaumbele hicho. 


Maeneo hayo ni:Uwekezaji katika mifumo ya kisasa ya kidijitali ili kuongeza ufanisi wa kiutendaji katika Vyama vya Ushirika, pamoja na Mamlaka za Usimamizi.


Kuharakisha mchakato wa uanzishwaji wa Benki ya Taifa ya Ushirika ili kuviwezesha Vyama vya Ushirika kupata Mikopo yenye Riba nafuu.


Kuhamasisha mfumo wa Ushirika kujiendesha kibiashara wenye kuaminika na shindani ukijikita kwenye kuongeza thamani ya uzalishaji katika Vyama; 


Kuboresha Sera, Sheria na usimamizi wa Ushirika ili kuchochea ukuaji na maendeleo ya Ushirika imara Tanzania; 


Kuhamasisha Ushirika kwenye sekta mbalimbali na makundi maalum ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wananufaika na mfumo wa Ushirika; 


Kuimarisha uwekezaji wa mali za Ushirika katika uzalishaji; 


Kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutatua changamoto zilizopo kwenye Ushirika.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI