Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi akionesha leo kwa waandishi wa habari hawapo pichani bunduki aina Gobore iliyokamatwa katika Oparesheni iliyofanywa mkoani hapa
JESHI la polisi mkoa wa Iringa limetaja mafanikio yaliyopatikana kati ya Julai 5 hadi Julai 12 mwaka 2023 kuwa mbali ya kukamata watuhumiwa wa makosa mbali mbali watuhumiwa 11 waliokamatwa na kufikishwa mahakamani walikutwa na hatia akiwemo Naftar Lyandala (40) mkazi wa Uhambingeto ambaye amehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la mauwaji .
Akitoa taarifa jana kwa waandishi wa habari kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Allan Bukumbi alisema kuwa mbali ya Lyandala kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa wengine ni Francis Masoud (41) mkazi wa Kitasengwa , Denis Mtega (31) mkazi wa Ilula Mtua na Emannuel Nzogela (29) mkazi wa Ipogolo kwa nyakati tofauti wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa ya kubaka.
Aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Godfrey Chengula (33) mkazi wa Isakalilo aliyehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kutoroka chini ya ulinzi , Batros Kipako (47) aliyehukumiwa mwaka mmoja jela kwa kosa la kupatikana na silaha aina ya Gobore , Musa Mtung'e (35) mkazi wa Idodi alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kujaribu kubaka ,Prudence Patrick (24) mkazi wa TRM KIhesa alihukumiwa kifungo cha miaka 7 kwa kosa la mauaji pamoja na Desderia Mbwelwa (52) mkazi wa Lumuli Ifunda aliyehukumiwa kifungo cha miaka 26 kwa kosa la shambulio la aibu dhidi ya mtoto .
Kamanda Bukumbi alisema Emmanuel Mahundi (31) mkazi wa kijiji cha Ibumu wilaya ya Kilolo alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka pamoja na fidia ya shilingi 500,000 huku Godi Kasungula (41) mkazi wa Ipilimo wilaya ya Mufindi akihukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha .
Pia alisema katika oparesheni ya kuthibiti magari yanayotembea usiku kwa kutozingatia sheria jeshi la polisi lilifanikiwa kukamata magari 12 kwenye oparesheni hiyo iliyofanyika mkoani hapa kati ya Julai 5 hadi Julai 12 mwaka huu na kuwachukulia hatua za kisheria madereva kwa kushindwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuendesha magari ya abiria bila leseni ya usafirishaji kukosa ratiba za safari na makosa mengeni ya kiusalama barabarani .
Aidha jeshi la polisi Agost 8 mwaka huu lilimkamata Jacob Mhanga (54) mkazi wa Kijiji cha Utiga mkoa wa Njombe akiwa na vipande saba vya meno ya Tembo katika nyumba ya kulala wageni iliyopo kijiji cha MBalamaziwa kata ya Kasanga wilaya ya Mufindi kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.
Bukumbi alisema katika misako mbali mbali inayoendelea jeshi la polisi kwa kushirikiana na askari wa Uhifadhi kwa kupokea taarifa fiche kupitia Raia wema Agost 6 mwaka huu majira ya saa moja usiku walifanikiwa kumkamata Mathias Malenga (37) mkazi wa kijiji cha Image Tarafa ya Mazombe wilaya ya Kilolo akiwa na silaha mbili ndani ya nyumba yake moja ikiwa ni Shortgun isiyo na namba ikiwa na risasi mbili na maganda matatu na nyingine ni Gobore moja na Goroli sita pamoja na mtego wa kuwindia wanyama kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani .
Kati hatua nyingine kamanda Bukumbi alisema kupitia oparesheni iliyofanyika Juni 7 hadi Julai 10 mwaka huu jeshi la polisi mkoa wa Iringa lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa tisa wa makosa mbali mbali ya kuvunja na kuiba ambao ni Samweli Malila mkazi wa Kinyanambo C Mafinga wilaya ya Mufindi , Fahamu Msisi (40) mkazi wa Mji Mwema Mafinga ,Satoki Sanga (50) mkulima wa Luganga ,Steven Peter (43) mkazi wa Mafinga , SAid Degele(24) mkazi wa Mwangata ,Joshua Elihuruma (42) mkazi wa Kitanzini na Goodluck Mpangile (25).
Alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na mali mbali mbali zi;nazodhaniwa kuwa za wizi ambazo ni pikipiki nne zenye namba za usajili MC 473 AAP na MC 294 DPG zote aina ya Haojue pia pikipiki aina ya SUNLG yenye namba Chasis LBRSPKB5509004894 na PIkipiki matairi matatu MC 724 DHJ.
Vitu vimngine walivyokamatwa navyo ni pamoja na TV moja aina ya EVVOL yenye S/N 0C15 na NM 1DK140985-00838,MN 32EV100,Laptop mmoja aina ya SnSV yenye S/N 0C15 na M/N 9461D2W jeki moja ya gari na spana mbali mbali pamoja na Extension Cable mbili ,Blankent moja ,magodoro mawili na vitu mbali mbali vya dukani kama Cherehani na vingine vingi .
Hata hivyo kamanda Bukumbi mbali ya kuwashukuru wananchi wanaoendelea kuchukizwa na watu wanaojikhusisha na uhalifu na matukio ya uhalifu bado aliomba raia kuendelea kutoa ushirikiano zaidi kwa jeshi la polisi kwa kuwafichua wahalifu na uhalifu .
0 Comments