Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
KATIKA Mwaka wa fedha 2023/2024, Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Manzigira Dar es salaam ( DAWASA) imejipanga kuendelea kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi kupitia utekelezaji wa miradi ya kimkakati saba ikiwemo wa bwawa la Kidunda, Mradi wa ujenzi wa Mtambo wa kuzalisha maji wa Rufiji.
Hayo yameelezwa leo Agost11,2023 Jijini Dodoma na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Kiula Kingu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi na kueleza kuwa ndani ya mwaka wa fedha 2022/23
Amesema miradi mingine ni wa maji Kwala, Mradi wa maji Mji wa Pangani Kibaha, Ujenzi wa mradi kutoka
Kimbiji-Kigambonihadi jirani naChuo cha Uhasibu T.I.A, Ujenzi wa mradi wa maji Kusini mwa Jiji la Dar es salaamna Mradi wa uchimbaji visima virefu tisaeneo la Kigamboni.
Amesema miradi hiyo itakayotekelezwa kwa jumla ya Tsh.Bilioni 425.9 ina inalenga katika kuongeza wingi wa maji yanayozalishwa na DAWASA,kuongeza uwezo wa kuhifadhi maji, kuimarisha mfumo wa usambazaji majina kuimarisha huduma katika maeneo ambayo hayana mtandao hasayale ya pembezoni
Aidha Kuhusu utekelezaji wa utunzaji wa mazingira alisema DAWASA imekuja na ubunifu wa kujenga mifumo na mitambo midogo midogo ya kuchakata majitaka inayojengwa maeneo ya pembezoni ambapo zaidi yalita 780,000 za
majitakazitakuwa zikichakatwa kwa siku.
"Miradi hii ambayo pia itajumuisha ujenzi wa vyoo vya umma 30, itasaidia kuongeza wigo waupatikanaji wa huduma hizi muhimu na
hivyo kuboresha usafi wa mazingira,"alifafanua Kingu
Aliongeza kuwa miradi hiyo itasaidia wananchi kupata huduma
za usafi wa mazingirakwa gharama nafuu karibu na maeneo wanayoishi.
" Wakandarasi wanaotekeleza miradi wanaendelea na ujenzi,gharama za miradi hii ni jumla yaTsh.bilioni 25.7na wanufaika wa miradi hii wanakadiriwa kufikia milioni1.8,"alisema
Na kuongeza Kusema "Miradi mikubwa iliyo tekelezwa na kukamilishwa 2022/23 ni pamoja na,mradi wa ujenzi wa mfumowa usamabzaji maji kati ya Bagamoyo hadimatenki yaliyopo jirani na Chuo kikuucha Ardhi, mradi wa maji Kigamboni, mradi wa maji Chalinze awamu ya tatu na mradi
wa maji Mshikamano,;
Mwingine ni mradi wa maji nje ya mtandao(unaohudumia mitaa 12), mradi wa Maji Mbezi Makabe,mradi wa maji Zegereni, Mradi wa maji Soga, Mradi wa maji Mbwawa na miradi ya maji 14 iliyotekelezwa chini ya programu ya lipa kwamatokeo.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa miradi hiyo ambayo ina uweo wa kuhudumia wakazi 722,308 katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani ilijengwa kwa gharama ya jumla shilingbilioni219.4.
0 Comments