Header Ads Widget

TANZANIA NA MALAWI KUSHIRIKIANA UZALISHAJI WA NISHATI


Na Fatma Ally - Matukio Daima App, Dar es Salaam.

Tanzania na Malawi zimesainiana makubaliano ya kushirikiano katika uzalishaji nishati ya mafuta, gesi ambapo makubaliano hayo yataleta tija kwa nchi zote mbili.


Aidha, makubaliano hayo ni sehemu ya mradi wa kikanda wa kuwa na gridi moja katika kanda hii ambapo miradi hiyo  itanufaisha nchi Tanzania na Malawi kwa sababu mahitaji ya umeme bado ni makubwa.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Nishati Januari Makamba mbele ya Mawaziri wa sekta hiyo kutoka Malawi amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya kufuatia maelekezo ya Marais wa nchi hizo, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Lazarus Chakwera.


Akizungumza katika hafla hiyo ya kusaini makubaliano hayo Waziri wa Nishati wa Tanzania January Makamba amesema makubaliano hayo pia yatahusisha ujenzi wa miundombinu ya umeme na ujenzi wa megawati 180 kwa kutumia maporomoko ya mto Songwe.


Aidha amesema kutakuwa na kamati ya pamoja ya mawaziri na kamati ya wataalam ambapo kila upande utateua wataalam na vikao vitaanza rasmi Oktoba mwaka huu.


"Maelekezo ya viongozi wetu Rais Samia Suluhu na Rais Chakwera walikubaliana tuongeze maeneo ya ushirikiano hasa eneo la nishati hivyo tunachofanya saivi ni utekelezaji wa maagizo yao" amesema Waziri Makamba.


Kwa upande wake, Waziri wa Nishati Malawi, Ibrahim Matola, amesema nchi nyingi Kusini mwa Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki bado hazina nishati ya kutosha hivyo ni muhimu kuwe na miradi mingi zaidi katika sekta hiyo.


"Makubaliano haya ni mwanzo wa safari yetu ya kushirikiana katika nyanja nyingi. Rais Samia na Rais Chakwera walikubaliana kushirikiana pamoja kwa manufaa ya mataifa haya. Ni muhimu tuwe na miradi mingi zaidi katika sekta ya nishati," amesema Matola.


Aidha, Rais Samia alifanya ziara nchini Malawi Julai 5, 2023 ambapo pamoja na mambo mengine viongozi hao walikubaliana kuendelea kushirikiana kwenye maeneo mbalimbali kudumisha uhusiano uliopo.


Nchi hizo pia zimekubaliana kushirikiana katika eneo la gesi ambapo Tanzania inatarajia kuuza gesi Malawi ambapo ongezeko hilo la nishati litawezesha kuongeza uzalishaji wa bidhaa Viwandani kwa bei nafuu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI