Header Ads Widget

MWANASHERIA DHIDI YA MKATABA WA BANDARI AKAMATWA MOROGORO.


Na Simon Joshua - Matukio Daima App, Morogoro.

Mwanasheria na wakili msomi Boniface Kanjunjule Mwabukusi amekamatwa na Jeshi la Polisi  Mikumi, Morogoro akiwa pamoja na Katibu wa Kanda wa CHADEMA, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali.


Inadaiwa kuwa walikuwa safarini kuelekea Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, watu waliojitambulisha kuwa ni Askari ndio wamewakamata pasipo kutaja kosa lao na wapi wanapelekwa zaidi ya kuambiwa ni Maelekezo kutoka Juu. Pia, vifaa vyao vya mawasiliano (Simu za mkononi) vimechukuliwa.


Mwabukusi, aliyeongoza kesi dhidi ya Serikali ya Muungano wa Tanzania kuhusu mkataba wa bandari unaodaiwa kununua bandari ya Tanzania kwa waarabu wa DP World (DPW), ni miongoni mwa wanasheria wa viwango vya juu sana nchini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI