Header Ads Widget

SERIKALI YAOMBWA KUONGEZA VYUO NA WATALAAMU WA ARDHI.


Na Chausiku Said-Matukio Daima App, Mwanza.

Serikali imeombwa kuongeza vyuo na watalaamu wa ardhi Nchini ili kuisadia jamii na kutoa elimu juu ya migogoro ya Ardhi na ujengaji holela wa makazi.


Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Ardhi mataji Athuman Nassoro wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika maonesho ya nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nyamhongoro Mkoani Mwanza.


Nassoro ameeleza kuwa wananchi bado wanauwelewa mdogo juu ya matumizi bora ya Ardhi hivyo elimu inatakiwa kuongezeka ili kupunguza  migogoro inayojirudiarudia hapa nchini.


Kwa upande mwingine Amesema kuwa chanzo kikubwa kinacho sababisha migogoro hiyo ni ununuzi wa Ardhi bila kupima na wazazi kutoandika urithi mapema wa umilikishaji wa eneo.


"Mara nyingi huwa tunaona kiwanja Kiko sehemu nzuri halafu hakuna ujenzi unaendelea mahali pale, kumbe unakuta wazazi walifaliki bila kuandika urithi Kila Mtoto anang'ang'ania ndio maana unakuta kajumba kabovu Kako eneo hilo miaka mingi bila kuendelea ujenzi" Alisema


Elizabeth Emmanuel na Michael Jackson ni baadhi ya wananchi waliofika katika Banda hili wameeleza kuwa migogoro ya Ardhi kwenye jamii bado ni mikubwa na watu wengi bado hawafahamu ni wapi watapata msaada.


Wameeleza kuwa hawakuwa na elimu ya kutosha juu ya ununuzi wa viwanja vilivyopimwa na namna ya kupata hati hali hiyo imekuwa ikisababisha ununuzi wa holelaholela wa viwanja


"Uwepo wa Banda hili litawasaidia watu wengi kufahamu ni namna gani mtu anaweza kupata kiwanja kilichopimwa na ukapatwa hati ya kiwanja chako na kuachana na viwanja ambavyo havijapimwa na kusababisha migogoro" Walisema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI