Header Ads Widget

RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO YA BARAZA LA MAWAZIRI.



Na Simon Joshua - Matukio Daima App, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri na Makatibu Wakuu. Katika mabadiliko hayo, Mhe. Rais ameanzisha nafasi ya Naibu Waziri Mkuu na kuifuta Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na badala yake kuunda wizara mpya mbili ambazo ni: 

Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Uchukuzi. Aidha, ameimarisha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuongeza nafasi ya Naibu Waziri na Katibu Mkuu watakaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki. Katika mabadiliko hayo, Mhe. Rais amemteua Naibu Waziri Mkuu, Mawaziri wanne (4), Naibu Mawaziri watano (5), Makatibu Wakuu watatu (3) na Naibu Makatibu Wakuu watatu (3). Vilevile, amewabadilisha wizara baadhi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu. Mabadiliko hayo ni kama ifutavyo:


A) Uteuzi wa Naibu Waziri Mkuu

Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko ameteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Katika nafasi ya Naibu Waziri Mkuu atakuwa anashughulikia Uratibu wa Shughuli za Serikali.


B) Uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri

1. Mhe. Jerry William Silaa, Mbunge wa Jimbo la Ukonga ameteuliwa kuwa

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi;

2. Mhe. Anthony Peter Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo ameteuliwa kuwa

Waziri wa Madini;

3. Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa aliyekuwa Waziri wa Ujenzi na

Uchukuzi ameteuliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi; 

4. Mhe. Innocent Lugha Bashungwa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi;

5. Mhe. Godfrey Msongwe Kasekenya aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi

6. Mhe. Alexander Pastory Mnyeti, Mbunge wa Jimbo la Misungwi ameteuliwa

kuwa Naibu Waziri wa Kilimo;

7. Mhe. David Mwakiposa Kihenzile, Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini

ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi;

8. Mhe. Judith Salvio Kapinga, Mbunge wa Viti Maalum (Ruvuma) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nishati; na

9. Mhe. Dunstan Luka Kitandula, Mbunge wa Jimbo la Mkinga ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.


C) Uhamisho wa Mawaziri na Naibu Mawaziri

1. Mhe. January Yusuf Makamba amehamishwa kutoka Wizara ya Nishati kwenda kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; 2. Mhe. Stergomena Lawrence Tax amehamishwa kutoka Wizara ya Mambo ya

Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenda kuwa Waziri wa Ulinzi na

Jeshi la Kujenga Taifa;

3. Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa amehamishwa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI; 

4. Mhe. Angellah Jasmine Kairuki amehamishwa kutoka Ofisi ya Rais -TAMISEMI kwenda kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii; na

5. Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kwenda kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo;

6. Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana amehamishwa kutoka Wizara ya

Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenda kuwa Waziri wa Katiba na Sheria; na

7. Mhe. Stephen Lujwahuka Byabato amehamishwa kutoka Wizara ya Nishati kwenda kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki atakayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki;

D) Uteuzi wa Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu

1. Prof. Godius Walter Kahyarara aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Geita ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi;

2. Mhandisi Cyprian John Luhemeja aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu);

3. Balozi Prof. Kennedy Gastorn ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki atakayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki;

4. Dkt. Ally Possi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi) ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya

Uchukuzi; 

5. Bw. Ludovick Nduhiye aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi) ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi;

na

6. Mhandisi Mwajuma Juma Waziri ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji.

E) Uhamisho wa Makatibu Wakuu

1. Prof. Jamal Adam Katundu amehamishwa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji;

2. Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe amehamishwa kutoka Wizara ya Afya

kwenda kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,

Wanawake na Makundi Maalum, na

3. Dkt. John Anthony Jingu amehamishwa kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwenda kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Afya.

Uteuzi huu unaanza leo, tarehe 30 Agosti, 2023. Viongozi walioteuliwa wataapishwa tarehe 1 Septemba, 2023 Ikulu Ndogo, Zanzibar. Saa 5:00 Asubuhi.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI