Header Ads Widget

MHANDISI MARYPRISCA AFUNGUA MAFUNZO ELEKEZI KWA BODI YA WAKURUGENZI RUWASA




.NAIBU Waziri wa Maji,  Mhandisi Maryprisca Mahundi ameeleza kufurahishwa na Kasi ya utekelezaji wa Miradi ya Maji nchini inayofanywa ma wakala wa Maji na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA)


Mhandisi Mahundi alitoa pongenzi hizo kwa Leo Mjini Iringa wakati akifungua Mafunzo elekezi kwa bodi ya wakurugenzi ya pili ya RUWASA 

Mhandisi Mahundi ambae alimwakilisha waziri wa Maji Jumaa Awesso alisema Wizara inajivunia utendaji Kazi wa RUWASA.

Kuwa Wizara wana amini kuwa maadili ya viongozi ni msingi muhimu wa uongozi bora na wenye tija kwa maendeleo endelevu.

"Hivyo, kwa kusimamia maadili, wajumbe wa bodi mnatakiwa kutekeleza majukumu ya kuiongoza RUWASA ni matarajio yangu kwamba mafunzo haya yatawapa mwanga na kuwaimarisha katika kuongoza kwa mfano na kuendeleza maadili ". Amesema

Pia Mahundi alisisitiza kwa Wajumbe wa Bodi kuwa wanahitaji kufahama na kusimamia viashiria hatarishi ili kuhakikisha ustawi na uendelevu wa taasisi. Wajumbe wa Bodi mnahitaji kuwa na ufahamu wa viashiria hatarishi.

Kuwa mafunzo haya yatawajengea uwezo wa kutambua, kusimamia, na kupunguza viashiria hatarishi kwa ustawi wa RUWASA.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi RUWASA Mhandisi  Ruth Koya alimpongeze Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa Mwenyekiti wa bodi ya pili ya RUWASA.

Vilevile ameishukuru Wizara ya Maji kwa ushirikiano mzuri wakati wa utekelezaji wa majukumu yake
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi Kulia akiteta jambo na Mwenyekiti wa bodi ya RUWASA Taifa Mhandisi Ruth Koya 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI