Header Ads Widget

NMB YAKABIDHI VIFAA MBALIMBALI KWA AJILI YA SHULE ZA SEKONDARI NA MSINGI MTAMA

 



NA HADIJA OMARY_ LINDI.....


BENKI  ya NMB Kanda ya kusini imekabidhi madawati, mabati, vitanda pamoja na kompyuta vyenye thamani ya zaidi ya milioni 30,000,000 kwa ajili ya shule tatu za Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi kama namna ya kurudisha faida waliyoipata kwa jamii 



Ghafla hiyo imefanyika jana August 9/2023 katika viwanja vya shule ya Sekondari Nyangao iliyopo Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi 



Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Meneja wa NMB kanda ya kusini Faraja Ng'ingo alisema vifaa hivyo vilivyokabidhiwa ni madawati 50 kwa ajili ya shule ya msingi Mmangawanga yenye thamani ya shilingi 4,900,000, Mabati 150 kwa shule ya msingi majengo yenye thamani ya shilingi 5,850,000 na vitanda 40 vya ngazi ( Double deckers) pamoja na kompyuta 10 kwa shule ya sekondari Mtama ambayo vina thamani ya shilingi 19, 800,000




Meneja Ng'ingo alibainisha kuwa Changamoto za sekta ya elimu Tanzania kwa Benki ya NMB ni jambo la kipaumbele na hiyo ni kutokana na ukweli kwamba Elimu ndio ufunguo wa maendeleo kwa taifa lolote hapa ulimwenguni 



" tunatambua juhudi za serikali ya awamu ya sita  chini ya mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kusimamia upatikanaji wa Elimu bora kwa nguvu zote kwa kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma hizi mjini na vijijini hatuna budi kuipongeza kwa hilo".


Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Lindi  Zainab Telack aliwapongeza NMB kwa hatua hiyo ya kurejesha kwa jamii huku akibainisha kuwa kitendo hicho ni cha Mfano na kwamba kinapaswa kuigwa na Taasisi zingine .



Amesema kitendo hicho kinarejesha furaha kwa jamii ambayo kwa kipindi kirefu watoto wao walilazimika kuishi nyumbani baada ya Bweni la shule yao kuunga kwa moto.


Mkuu wa shule ya Mtama sekondari Asha Namjupa alisema kuwa tangu 2019 baadaya ya Bweni la shule hiyo kuungua Moto Matokeo ya wanafunzi wa kike yamekuwa yanadorora.


Amesema msaada huo utakuwa chachu ya kusaidia kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa kike Shuleni hapo.



"Mwaka 2020 wanafunzi wa kike waliohitimu ni 57 waliopata daraja 0 ni mmoja, 2021 wanafunzi wakike waliohitimu ni 67 waliopata daraja 0 saba, mwaka 2022 wasichana 59 waliopata daraja 0 ni tisa hii inajionyesha wazi kuwa  kuna mtiririko wa kufeli kwa watoto wa kike"



Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wengine Sophia Rajab wanafunzi wa kidato cha tatu shule ya Sekondari Mtama   aliishukuru Benki ya NMB kwa msaada walioutoa na kwamba itaongeza chachu kuendelea kusoma kwa bidii ili kupata mayokeo mazuri.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI