Na Gift Mongi MATUKIO DAIMA APP MOSHI
Ni ziara zenye tija kwa taasisi mbalimbali na wananchi katika jimbo la Moshi Vijijini linalowakilishwa na Prof Patrick Ndakidemi ambapo ameendelea kukagua miradi mbalimbali lakini pia kujiridhisha na maendeleo yanayofanyika.
Ipo miradi ambayo inatekelezwa na serikali kuu lakini pia ile ambayo wananchi wenyewe wamehamua kujitolea katika utekelezaji wake lengo kuu haswa likiwa ni kuchagiza maendeleo katika jimbo hilo.
Mapema mwezi agusti 2023 mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi alitembelea na kukagua maendeleo ya Chuo cha Kibosho Vocational Training Center kilichoko katika tarafa ya Kibosho, Halmashauri ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro.
Katika ziara hiyo Prof. Ndakidemi alitembea na kujionea miradi ya kilimo na ufugaji inayotekelezwa hapo chuoni.
'Yaani ninaridhishwa kwa haya yanayoendelea hapa chuoni mimi binafsi nawaunga mkono katika kuzalisha wataalamu wapya katika sekta hii yenye uhitaji mkubwa katika ustawi wa taifa letu'anasema
Aidha Prof Ndakidemi alifanya ziara katika chuo hicho ikiwa ni mwaliko wa mkuu wa chuo Daniel Mboya kutaka kuona jitihada mbalimbali zinazofanyika katika kukuza sekta ya kilimo na ufundi kwa ujumla.
Aidha chuo hicho kinakabiliwa na uhaba wa fedha jambo linalopelekea kukwama kwa ujenzi wa baadhi ya miundombinu kama alivyoeleza mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho Thomas Kimboka.
'Tuna ukata wa fedha jambo linalokwamisha kutofanya ujenzi wa baadhi ya miundombinu na hakika tukipata fedha huenda tukawa na maendeleo zaidi ya hapa nadhani ujio wako huenda ikawa ni neema kwetu leo'anasema
Kutokana na umuhimu wa chuo hicho hususan kwa vijana wanaohitimu katika shule mbalimbali katika jimbo hilo Prof Ndakidemi alishauri kuwa uongozi uitishe harambee na kuwakaribisha wadau mbalimbali ili kuchangisha fedha za kukamilisha ujenzi huo.
'Itisheni harambee na sisi wadau tupo mtushorikishe ili tuweze kupata fedha za ujenzi wa chuo hiki muhimu katika eneo letu hili ambalo pia vijana wetu watakuja kupata ujuzi na kujikomboa wao wenyewe'anasema
Chuo cha Kibosho Vocational Training Center kinamilikiwa na wananchi wa Tarafa ya Kibosho yenye kata sita.
0 Comments