Na Gift Mongi MATUKIODAIMA APP MOSHI
Sasa rasmi mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi(UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirima ameuaga ukapera.
Ilikuwa siku nzuri hapa maeneo ya Kilihome akisherehekea maamuzi haya yakubadilishwa jina na kuitwa mume bà dala ya yale majina 'baby,my,honey'
'Tumefurahi kumuoma kijana mwenzetu akisherehekea ndoa yake na Mungu amtangulie katika haya majukumu mazito'anasema Geofrey Munisi
Sherehe hii ya aina yake imefanikiwa kuwakutanisha watu wa kada tofauti tofauti ambapo pia ilifana mithili ya ujio wa Masiya ambapo ilikuwa pia ni gumzo.
'Ndio tumefurahi kumuona mwenyekiti wetu anauaga ukapera ni jambo zuri sana tumtakie kila la kheri katika maisha haya mapya anayoyaanzisha'anasema
Wakili Emanuel Mlaki anasema ndio ni jambo jema na hivyo mwenyekiti huyo ameonyeshwa njia kwa vijana wanaogopa ndio
Anasema kuwa ndoa ni heshima kwa jamii lakini pia ni Baraka kutoka kwa Mungu na kuwa lazima iheshimiwe.
'Vijana wengi wanaogopa ndoa na hili lazima tuweke sawa ni mpango wa Mungu na uzuri lipo katika maandiko lazima tuheshimu'anasema
Fatuma Mwende anaongeza mwenyekiti huyo kwa kufunga ndoa na kuwa hii inatoa taswira ni jinsi gani kijana anatakiwa kuwa picha ya anaowaongoza.
'Ukiona kijana anafikia hatua ya kuwa na mwenzi ndani yaani mke uje ameshakomaa kiakili tayari hivyo hata maamuzi yake yatakuwa na busara'anasema
Mwisho
0 Comments