Header Ads Widget

MAISHA MAPYA YA NDOA MWENYEKITI UVCCM MOSHI VIJIJINI FURAHA TUUU..



Na Gift Mongi MATUKIODAIMA APP MOSHI

Huenda ni mstari mpya na taswira mpya ya kimaisha anayajenga sasa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi(UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirima baada ya kuuaga rasmi ukapera hapo agusti 12.2023.

Naam ni katika mazingira ambayo kila mwanadamu anayatamani Kwa kuitwa mume au mke ambapo rasmi sasa mwenyekiti huyu amevishwa majukumu ya kuwa mume tangu jana.

'Sisi vijana tunafurahia kumuona mwenzetu kapiga hatua na kupata jiko huenda anatuhamasisha na sisi kufanya hili jambo bora mbele ya Mwenyezi Mungu"Clifford Shoo

Bi Regina Chonjo ambaye ni mjumbe wa kamati ya siasa(CCM) wilaya ya Moshi Vijijini anasema hakika limekuwa jambo jema Kwa mwenyekiti huyo kuwa na majukumu hivi sasa.


'Simaanishi alikuwa hana majukumu bali yale yanayoendana na familia sasa hivyo tuliongea naye tayari anaguswa pande zote kama kijana,mzazi,mlezi,kada nk 'anasema

Ilikuwa ni sherehe ya aina yake ambayo ilifurika watu na wageni mbali mbali wakiwemo makada wa chama cha mapinduzi(CCM)waliomsindikiza kada mwenzao katika tukio hilo muhimu.

Hata hivyo katika ukumbi huo wa Kilihome ambapo shughuli hiyo ilitamatikia vijana wengi waliohidhiria tukio hilo wameoneshwa kugongwa moto yao na kuhamasika kuachana na ukapera sasa.

'Mimi ni nani kama mwenyekiti kaamua kuaga ukapera nampingaje sasa huu ndio uongozi sahihi tulikuwa tunataka'anasema Emanuel Mallya kutoka kata ya Kibosho  

Anasema kuwa ndoa ni heshima kwa jamii lakini pia ni baraka kutoka kwa Mungu na kuwa lazima iheshimiwe Kwa kuwa imehakalishwa duniani na mbinguni.

'Vijana wengi wanaogopa ndoa na hili lazima tuweke sawa ni mpango wa Mungu na uzuri lipo katika maandiko lazima tuheshimu'anasema

Fatuma Mwende anampongeza mwenyekiti huyo kwa kufunga ndoa na kuwa hii inatoa taswira ni jinsi gani kijana anatakiwa kuwa picha ya anaowaongoza.

'Ukiona kijana anafikia hatua ya kuwa na mwenzi ndani yaani mke uje ameshakomaa kiakili tayari hivyo hata maamuzi yake yatakuwa na busara'anasema

Mwisho




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI