Header Ads Widget

VIJANA WA ITIFAKI UVCCM MOSHI VIJIJINI WAONGOZA MAZISHI YA KATIBU WA CCM KAHE...

 Na Gift Mongi

MATUKIO DAIMA APP MOSHI


Aliyekuwa katibu wa chama cha mapinduzi (CCM)tawi la Mikaeni kata ya Kahe Mashariki Ashura Hamisi Mchomvu hatimaye amepumzishwa katika nyumba yake ya milele nyumbani kwake mnamo tarehe 29.08.2023.

Katika safari hiyo ya mwisho ya kiongozi huyo viongozi mbalimbali walijitokeza kumsindikiza kiongozi na kada wa Chama cha Mapinduzi katika safari yake ya mwisho.

Katika kumsindikiza aliyekuwa kiongozi mwenzao viongozi waliobahatika  kushiriki ni mwenezi wa CCM wilaya ya Moshi Vijijini  Hussen Jamal ,mwenyekiti  Wa UVCCM wilaya ya moshi Vijijini COMRADE Yuvenail Shirima, Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Moshi Vijijini ,Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Moshi Vijijini , Ndugu  diwan


i wa Kahe Mashariki Camilius  Mbando Diwani wa Njiapanda Loveness Mfinanga Mwenyekiti wa CCM kata na kamati ya Siasa kata Viongozi mbalimbali wa Baraza la UVCCM Wilaya na Viongozi mbalimbali wa CCM na serikali Wilaya kata kijiji na Vitongoji

Wa mujibu wa taarifa ya mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Moshi Vijijini maheremu Ashura Mchomvu amezikwa kwa heshima zote za chama cha Mapinduzi CCM, Vijana wa Itifaki wameongoza shughuli zote na kufanikisha kumpumzisha marehemu Ashura.

'Kwa namna ya kipekee nawashukuru sana vijana wa Itifaki viongozi mbalimbali kwa ushirikiano mkubwa mlioonesha kwa familia ya Marehemu Ashura katika Kumuhifadhi.

Mungu awabariki wote Mlioshiriki'anaeleza Yuvenail Shirima Mwenyekiti wa UVCCM Moshi Vijijini 

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI