Header Ads Widget

MAREKANI YAUA WANAMGAMBO 13 WA AL SHABAAB.


Na Simon Joshua - Matukio Daima App, Somalia.

Jeshi la Marekani limesema linaamini kwamba limewaua wanamgambo 13 wa al-Shabaab kusini mwa Somalia katika kile ilichokiita shambulizi la pamoja la kujilinda kufuatia ombi la serikali ya Somalia.


Kamandi ya Jeshi la Marekani Barani Afrika (AFRICOM) imesema ilifanya shambulizi la anga siku ya Jumamosi (Agosti 26) dhidi yakundi la al-Shabaab karibu na mji wa Seiera ulioko umbali wa kilomita 45 kaskazini magharibi mwa Kisimayo baada ya kuombwa na serikali.


Serikali ya Somalia na washirika wake walianzisha kampeni mwaka uliopita ya kuwafukuza wanamgambo hao wenye mahusiano na kundi la kigaidi la al-Qaeda, ingawa kundi hilo limeendelea kufanya mashambulizi makubwa.


Jeshi la Somalia na washirika wake siku ya Ijumaa walifanikiwa kuukamata mji wa El Buur, ambao ni ngome kuu ya al-Shabaab katika eneo la katikati mwa nchi hiyo, hii ikiwa ni hatua muhimu katika kampeni hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI