Header Ads Widget

KWA MARA YA KWANZA UMEME WAWASHWA KATA YA LUGENGE NJOMBE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Kwa mara ya kwanza wakazi wa vijiji vinne vya Kata ya Lugenge halmashauri ya mji wa Njombe Mkoani Njombe wamepata nishati ya umeme baada ya kusubiri kwa miaka mingi sasa.


Vijiji hivyo vya Kiyaula Kisilo,Lugenge na Idihani vimekuwa gizani tangu vianzishwe na sasa serikali kupitia mradi wa nishati vijijini REA imewasha umeme huo kwa mara kwanza na historia kuandikwa katika serikali ya awamu ya sita.



Chama cha mapinduzi ccm wilaya ya Njombe Chini ya mwenyekiti wake Justin Nusulupila kimeshuhudia zoezi la uwashwaji umeme huo na kwamba wananchi wa kata hiyo wamekuwa mwiba mkali katika kushinikiza kupatikana kwa umeme.


Neema Lyakulwa ni afisa uhusiano wa shirika la Umeme Tanzania Tanesco mkoa wa Njombe kwa niaba ya meneja wa Shirika hilo amesema wakati umeme huo ukiwashwa katika kata hiyo wananchi wanapaswa kuonyesha kwa vitendo kuunganisha kwenye nyumba zao ili uwasaidie.



Diwani wa kata ya Lugenge Filoteus Mligo ambaye ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe amesema wamelazimika kuwashia umeme huo katika kijiji cha Idihani ambacho kipo mwishoni mwa kata hiyo kutokana na laini kuu kuanzia katika kijiji hicho.


Wakazi wa kata ya Lugenge akiwemo Lukiel Mwalongo,Anjelwis Mgungilwa mkuu wa shule ya sekondari mgola na mwenyekiti wa CCM kata ya Lugenge wameonesha kufurahishwa na hatua ya umeme kufika kwa mara ya kwanza kijiji humo huku wakiomba kasi ya kusambaza katika vitongoji vingine iongezeke.



Serikali ya awamu ya sita iliahidi kupeleka nishati ya umeme katika vijiji vyote nchini ili kurahisisha huduma za kijamii na  mawasiliano na kukuza uchumi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI