Header Ads Widget

ULEGA AMSHUKURU RAIS KWA FEDHA NA ENEO LA KUJENGA SHULE VIKINDU

 



Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia eneo katika msitu wa Hifadhi wa Vikindu na  fedha za kujenga Shule ya msingi na Sekondari katika eneo hilo.


Amesema hayo katika mkutano wa hadhara uliohusisha Wananchi wa Kata nzima ya Vikindu katika viwanja vya Standi ya Vikindu Mkuranga mkoani Pwani wakati akizungumza na Wananchi kwenye Ziara yake jimboni humo.


Ulega amesema wao waliomba kibali cha kubadilisha matumizi ya sehemu ya eneo la Msitu wa  Vikindu ili Wananchi waweze kupata eneo la huduma za jamii ikiwemo kujenga shule ya Sekondari na Msingi kwani watoto wadogo walikuwa wakitembea umbali mrefu kufuata shule lakini Rais amewapatia eneo na fedha za kujenga shule hizo.



"Sisi tuliomba eneo la msitu tujenge shule lakini Mama yetu kwa upendo mkubwa ametupatia fedha za kujenga shule ya Sekondari na ya msingi sio jambo dogo jamani, shule ya Sekondari kidato cha kwanza wameshaanza kusoma na hii msingi sio muda mrefu wataanza kusoma" 


Amesema Ujenzi wa Shule ya msingi unaoendelea Serikali imetoa Shilingi milioni 400 ambayo ujenzi wake upo hatua za mwisho kukamilika na Ujenzi wa Shule ya sekondari ni kwa fedha za Uviko 19 ambapo milioni 160 zimejenga madarasa 8 ambayo tayari Wanafunzi wameanza kusoma.


"kijiji wazazi pia wamekuwa wakigharamika kulipa boda boda ya zaidi ya shilingi 6000/- kwa siku ili waende shule au Watoto wao watembee umbali huo wa kilomita kumi kufuata Shule" amesema Ulega.


"Kwani kati yetu kuna aliyetoa shilingi Kumi yake katika ujenzi huu? Hatuna cha kumlipa Mama huyu bali ni kuendelea kumuombea Dua Mungu amlinde na kumuepusha na Kila shari za walimwengu" amesema Ulega huku akiwa ameinua mikono juu na macho juu.


Amesema "mwaka 2018 alikuja hapa Waziri wa Utalii Jumanne Magembe akatukabidhi kibali cha kubadilisha matumizi ya sehemu ya eneo la Msitu wa Vikindu na tayari tumepata shule mpya za sekondari na msingi na Wanafunzi wameanza kusoma ni jambo kubwa mno"



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI