Na Fadhili Abdallah - Matukio Daima App, Kigoma.
Timu ya soka ya mashujaa ya mkoani Kigoma imetambulisha kikosi cha wachezaji, benchi la ufundi na uongozi wa timu hiyo kwa wapenzi wa soka mkoani Kigoma huku KOCHA wa timu hiyo Abdallah Barres akijigamba timu yake kufanya vizuri kwenye msimu huu wa ligi mkuu ya NBC ambayo inatarajia kutumia vumbi kuanzia jumatano wiki hii.
Akizungumzia kwenye uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika baada ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya Inter stars ya Burundi kocha huyo wa Mashujaa alisema kuwa usajili ambao timu hiyo imeufanya unampa nafasi ya kuona namna ambavyo timu hiyo itafanya vizuri.
Pichani: Kocha wa timu ya Mashujaa Abdallah Barres (Mwenye kofia) akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Alisema kuwa wiki mbili ambazo amekaa na timu hiyo kwenye Pre Season vsiwani Zanzibar anaiona timu hiyo kwenye mafanikio msimu huu na haitakuwa timu yenye historia ya kupanda daraja na kushuka kwa msimu mmoja.
Barres alisema kuwa bado anahitaji muda zaidi wa kukipika kikosi hicho lakini mchezo wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya klabu Bingwa ya Burundi Inter Stars imempa nafasi ya kuwatathimini baadhi ya wachezaji wake ili kupata kikosi cha kwanza.
Akizungumzia mchezo wa fungua Dimba dhidi ya Kagera Sugar unaotarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma Jumatano hii Kocha huyo wa Mashujaa anaamini itampa changamoto kubwa ili kupata matokeo kuweka imani wa malengo yake ya kufanya vizuri msimu huu wa ligi.
Pichani: Wachezaji wa timu ya Mashujaa wakizunguka uwanja kusalimia wapenzi wa timu hiyo wakati wa utambulisho wa uongozi,benchi la ufundi na wachezaji kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Akizungumzia mchezo wa fungua Dimba dhidi ya Kagera Sugar unaotarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma Jumatano hii Kocha huyo wa Mashujaa anaamini itampa changamoto kubwa ili kupata matokeo kuweka imani wa malengo yake ya kufanya vizuri msimu huu wa ligi.
Baadhi ya wapenzi wa soka wa mjini Kigoma waliohudhuria mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Mashujaa na Inter Stars ya Burundi na kutoka suluhu ya bao 1-1 walisema kuwa wamekiona kikosi na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo na kwamba wanaamini mabadiliko ya usajili yaliyofanyika yatakipa kikosi hicho nafasi ya kufanya vizuri msimu huu.
Samuel Laurent mkazi wa Mwasenga mjini Kigoma alisema kuwa sehemu kubwa ya wachezaji wa timu hiyo wameonyesha uwezo wa kuhimili mikiki mikiki ya ligi kuu kutokana na wachezaji waliosajiliwa kuwa wazoefu na ligi hiyo.
0 Comments