Header Ads Widget

MBUNGE ESTHER MALEKO "SERIKALI INAANDAA MPANGO MPYA WA JINSI YA KUKOPESHA MAKUNDI MAALUM"

 


NA WILIUM PAUL, MOSHI.

 

MBUNGE wa viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Esther Maleko amesema kuwa kwa sasa Serikali inatengeneza utaratibu mzuri wa kutoa mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ili uweze kuwafikia walengwa.

 

Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa kata ya Mamba kusini Jimbo la Vunjo wilayani Moshi ambapo alisema kuwa Serikali ilikuja kubaini fedha hizo zilikuwa zikitolewa kwa ujanja ujanja bila kufikia wale waliokuwa wakilengwa.

 


“Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusiana na kunyimwa mikopo hii na wakati mwingine zimekuwa zikitolewa kwa upendeleo ndio maana serikali ikaamua kuzuia kwanza kwa muda ili kutafuta njia nzuri ambayo itatumika ili walengwa wanufaike nazo” alisema Mbunge Esther.

 

Alisema kuwa, Serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi inataka kuona wananchi wote wananufaika bila kuangalia kipato cha mtu na kuwataka kuwa wavumilivu wakati serikali itakapokuja na mpango mzuri wa kukopesha mikopo hiyo isiyo na riba.

 


Mbunge huyo alisema kuwa, CCM inamkata na wananchi katika kuwatumikia hivyo itaendelea kusogeza huduma za kijamii karibu zaidi na wananchi.

 

Alisema kuwa, maendeleo katika jimbo la Vunjo yalikuwa yamelala kwa miaka 20 iliyopita lakini tangu Mbunge wa jimbo hilo atokane na CCM ambaye ni Dkt. Charles Kimei miradi mbalimbali ya maendeleo imeanza kutekelezwa kwa vitendo.

 


Aidha Mbunge huyo alisema kuwa, kumekuwepo na matukio ya ukatili dhidi ya watoto na wanawake na kutumia mkutano huo kuwaonya wananchi kuendelea kukemea vitendo hivyo na kuwaibua wale wote wanaofanya ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

 

Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi vijijini, Ramadhani Mahanyu alisema kuwa, wapo baadhi ya watu wameanza kupitapita na kuomba kuchaguliwa wawe Madiwani na Mbunge katika kata mbalimbali na kuwataka wananchi kuwapuuza.

 


“Kwa sasa tunaye Mbunge na Madiwani wa kata na viti maalum na wanafanya kazi nzuri mnaziona tuwaungeni mkono ili lengo la serikali pamoja na wao litimie hao wanaopitapita huku wapuuzeni” alisema Mahanyu.

 

Mwisho…

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI