Na,Jusline Marco;Arusha
Kamati za ufundi za Umoja wa Posta Afrika zimetakiwa kujadili masuala mbalimbali yanayohusika na mashirika ya posta barani Afrika ili kuendelea kuwa na tija katika kufikisha huduma kwa jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari baada kufungua Mkutano wa 41 wa Baraza la Utawala la Umoja wa Afrika PAPU ,Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Selestine Kakele amesema kamati hizo zimekutana kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kuendesha sekta hiyo na kuandaa ripoti itakayowasilishwa katika baraza hilo.
Aidha amesema baada ya kuandaliwa kwa ripoti hiyo,mapendekezo yatawasilishwa kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa maamuzi ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kiutendaji wa PAPU.
Aidha Kakele amesema kuwa mikutano hiyo ni muhimu katika uendeshaji wa sekta hiyo kwani ndipo mahali ambapo maamuzi ya msingi ya kibajeti naya kisera yanafanyika na sekretariet kupewa jukumu la kusimamia utekelezaji wake.
Ameongeza kuwa maendeleo ya teknolojia yanayoendelea yatumike kama fursa katika sekta ya Posta Barani Afrika hususani katika kukuza uchumi ambapo Tanzania kupitia Shirika la Posta Tanzania tayari limeanzisha husuma hiyo ili kwwnda sambamba na maendeleo ya teknolojia.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja Afrika ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Posta, Madagascar Bwn.Richard Ranarison ametaka vikao hivyo kufanyika kwa weledi ili kuhakikisha malengo ya kukuza sekta za Posta Barani Afrika yanafikiwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za mawasiliano kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mulembwa Munaku amesema katika kamati hizo ipo ambayo itaangalia uendeshaji na matumizi ya teknolojia,kamatibya kuangalia mikakati mbalimbali ya kuhakikisha mashirika ya posta yanaendelea kufanyakazi kwa ufanisi mkuwa,kamati ya kuangalia masuala ya sera pamoja na kamati ya kuangalia fedha na rasilimali watu.
Sambamba na hayo amesema kuwa mashirika ua posta yanamchango mkubwa katika matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano ili kuhakikisha yanaendelea kutoa huduma katika mazingira ya sasa.
0 Comments