NA THABIT MADAI- ZANZIBAR
WATOTO katika Kijiji cha Kidagoni na Kigongoni Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja wanalazimika kutembea Umbali wa zaidi ya Kilomita Mbili kwenda Shule kutokana na Vijiji hivyo kutokuwa na Shule hali inayopolekea kuwepo kwa Viashiria vya Udhalilishaji na Elimu kuwa Duni katika Vijiji hivyo.
Kutokana na Hali hiyo inapelekea kuwepo kwa tatizo la Utoro kwa Wanafunzi na Wanafunzi wengine kukatisha masomo na kufanya Elimu kuwa Duni katika Vijiji hivyo.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari Wananchi katika Vijiji hivyo wamesema kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni Miondombinu ya Barabara kuwa mibovu na watoto wanatembea umbali mrefu kufuata Shule na kuimba Serikali kutatua changamoto hizo.
"Hapa kijijini kwetu, tunakabiliwa na Changamoto nyingi sana ambazo zinarudisha nyuma maendeleo kubwa kuliko zote ni watoto wetu wanatembea umbali mrefu kufuata Shule pamoja na barabara kuwa mbovu," Amesema Ali Simai Silima.
Nae, Kirufi Ali Ame amesema kuwa, Adha hiyo ya kufuata Umbali Mrefu Shule inapekelea Wazazi kuwa na Wasisi kwa Watoto wao kutokea vitendo vya Udhalilishaji na Ukatili wa kijinsia.
"Kiukweli watoto Wetu wanapokuwa wanakwenda shule sisi huwa katika Roho juu maana hatujui huko njiani watakumbana na kitu gani maana ni umbali mrefu na Pori," ameeleza Kirufi.
Nae Asha Haji ambae ni Mwanafunzi katika Shule ya Kidagoni Msingi ameeleza kuwa tatizo la umbali Mrefu kufika Shule linawakosesha baadhi ya Masomo hali inayopelekea kuwa nyuma.
Mapema Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kidagoni Msingi Machano Khamis Machano amesema Umbali wa Shule pamoja na Ubovu wa Barabara unapeleka Utoro Sugu ambapo zaidi ya Wananfunzi 30 hadi 50 kwa Siku.
"Kiukweli adha hii imekuwa Kero kubwa kwetu maana nimezalisha tatizo la Utoro Sugu kwa Vijana wetu, Wanafunzi zaidi 20 hadi 50 hawafiki skuli huishia mwituni huko," ameeleza mwalimu.
Amesema kutokana na tatizo hilo kumekuwepo viashiria vya vitendo vya Udhalilishaji kutokana na Watoto wanatembea umbeli mrefu.
Kwa upande wake, Sheha wa Shehia ya kidagoni Vuai Mtosho bure ameiomba Serikali kuwezesha Kumalizia Ujenzi wa mabanda ya Madarasa aliouanzisha ili kuondokana na Kero ya Wanafunzi kutembea Umbali Mrefu kufuata Huduma ya Shule.
"Mimi na Wananchi wenzangu tumeamua kuanzisha ujenzi wa Mabanda ya Shule ili kuondoa changamoto hii inayowakabili vijana wetu hiyo naomba Serikali kuu iweze kutusaidia Kuondokana na Changamoto hii," amesema sheha.
Nae Mwanaharakati na Mratibu wa Mradi wa kuwawezesha Wanawake kushika Uongozi Kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Mariam Ame, amesema lengo la ziara hiyo kwa Wanahabari kuibua changamoto zinazoikabili jamii ili kupatiwa Ufumbuzi.
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tamwa kimeandaa ziara ya kihabari katika vijiji hivyo lengo ni kuangalia utekelezaji wa haki za Kidemokrasia.
0 Comments