Na Thabit Madai - Matukio Daima App, Zanzibar.
KUFUATIA Uteuzi wa Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Uchaguzi Zanzibar, Chama cha ACT Wazalendo kimesema kwamba, Kimepokea na kurudhishwa na Uteuzi huo na kuwataka kufanya Kazi kwa Weledi na kuzingatia Maslah ya Zanzibar.
Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari leo katika Ofisi Kuu za ACT Wazalendo Zanzibar Katibu wa Habari,Uenezi, Mahusiano ya Umma Salim Bimani amesema kwamba Chama kinawapongeza wateule wote na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia Maslahi Mapana ya taifa.
Amesema kuwa, Tume mpya ina Makamishna ambao ni wanasheria wazoefu na Weledi katika kuendesha uchaguzi.
"Tunawapongeza kwa dhati wote walioteuliwa kwa kupewa imani hiyo kubwa, ACT Wazalendo kinawatanabaisha kwamba ni watumshi wa Wananchi hivyo wajibu wao kuangalia maslah ya Zanzibar mbele," amesema.
Aidha Chama hicho kimewaomba Wananchi wote visiwani Zanzibar kuwaunga mkono na kushirikiana nao katika utekelezaji wa Maukumu yao ya kila siku.
"Tunaamini utendaji wenye uadilifu wa tume ya Uchaguzi utawezesha juhudi zinazoendelea za Mazungumzo ya kuleta mageuzi ya masuala mbalimbali ya mfumo wa uchaguzi, kidemokrasia, utawala wa sheria na utawala mwema kwa nia ya kuleta maridhiano endelevu." ameeleza.
Katika hatua nyingine Katibu huyo amewaeleza waandishi wa Habari kuwa Chama cha ACT Wazalendo kimejipanga vyema na Uchaguzi Mdogo katika Jimbo na Wadi zilikuwa Wazi.
Rais Dkt Husein Mwinyi Agost 24 amefanya uteuzi kwa viongozi na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ZEC ambao anatarajiwa kuwaapisha Agost 28 mwaka huu.
0 Comments