NA CHAUSIKU SAID_MATUKIO DAIMAAPP MWANZA
Mkurugenzi wa Kampuni ya cheza kidance intertement Mkoani Mwanza Bernard James ameandaa hafla ya kuwakutanisha wanandoa na wasio na ndoa ili kutatua changamoto ya Mmomonyoko wa maadili kutoka Kwa vijana wanaojihusisha na vitendo vya ulawiti, ushoga pamoja na mapenzi ya jinsia moja kutokana na utandawazi.
Amesema kuwa ameamua kufanya hafla hiyo ili kuyakutanisha makundi yaliyoko kwenye ndoa ,wanaotarajia kuingia kwenye ndoa pamoja na ambao hawapo kwenye ndoa ili kuondoa tatizo linalosababisha Mmomonyoko wa maadili katika Familia.
Bernard amesema kuwa Kuna baadhi ya mambo ambayo familia ikizingatia yataleta ustawi mzuri katika jamii na Mmomonyoko wa maadili hautakuwepo hususani Kwa vijana.
"Kuna utafiti mmoja umefanywa na gazeti moja hapa Nchini Tanzania Kila baada ya saa moja ndoa 13 zinakuwa kwenye migogoro katika familia na takribani zaidi ya Asilimia 53 ya vijana walio na sifa ya kuoa na kuolewa hawajaingia kwenye ndoa"Alisema Bernard.
Hata hivyo ameeleza kuwa watu wakifanya uamuzi nzuri wa kuchaguana na kuingia kwenye ndoa na kushirikiana kwenye mambo ya Msingi katika malezi na matatizo ya Mmomonyoko wa maadili hayakuwepo kwenye jamii.
Happiness Mtani ambaye ni mdhamini wa tamasha hilo amesema kuwa uwepo wa hafla hiyo utawasaidia watu katika kujenga familia iliyo Bora na salama.
" Zamani ulikuwa ukikataa kuishi na watu ulikuwa unaonekana una roho mbaya kadili siku zinavyozidi kwenda vitendo vya ulawiti vinazidi kuongezeka Kwa kufanywa na ndugu tunaoishi nao" Alisema Happiness.
0 Comments