Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
TUME ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imefadhili Mradi wa utafiti wa Somo la hisabati hapa nchini lengo likiwa ni kumaliza tatizo hilo hasa kwa wahitimu wa Darasa la saba na kidato Cha Nne.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Dkt.Amos Nungu ameyasema hayo leo jijini hapa amesema kuwa imeidhinisha miradi miwili (2) kwa thamani ya TZS 120M kila mradi.
Dkt.Nungu amesema utekelezaji wake pia unahusisha watafiti kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini na itafanyika ndani ya miaka miwili, sasa ipo hatua ya kusaini mikataba.
"Somo la hisabati Bado linaonekana ni changamoto kwani matokeo yake yamekuwa mabaya Kwa kidato Cha nne na Darasa la nne hivyo Kwa kuondoa tatizo Hilo sisi kama Tume tumeidhinisha miradi miwili ambayo kila mmoja thamani yake ni milioni 120,"amesema Dkt.Nungu
Dkt.Nungu amesema Miradi mingi ya utafiti hufadhiliwa kwa kipindi cha miaka miwili hadi mitatu. Kwa sasa ipo miradi kadha inayoendelea na ipo hatua mbalimbali ambayo Serikali ilifadhili kupitia COSTECH.
Michache katika miradi hiyo ya utafiti inayoendelea katika hatua mbalimbali za utekelezaji na Tume inafanya ufuatiliaji ni pamoja na ile inayohusu kuboresha maabara za utafiti kwa ukarabati na ununuzi wa vifaa vya kisasa ikiwemo.
Katika kuratibu, kukuza na kuendeleza utafiti, baadhi ya shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na Kuibua na kufadhili miradi ya kimkakati ambayo michakato imefanyika tayari na sasa ipo hatua ya mikataba ikiwemo Kuyaelewa na kuyatumia vema mapinduzi ya nne ya Viwanda ndiyo mwelekeo kwa dunia nzima.
Dkt.Nungu amesema Serikali kupitia COSTECH imeidhinisha jumla ya miradi saba (7) kwa thamani ya TZS 150M kila mradi. Miradi hii itafanyika ndani ya miaka miwili na inahusisha watafiti na wabunifu kutoka sekta zote, public and private.
Amesema COSTECH inaendelea kuimarisha mfumo wa ubunifu nchini kwa kuanzisha au kutoa usaidizi kwa vituo mbalimbali vya ubunifu (intemediaries) ili kuwafikia na kuwahuduma wabunifu kiurahisi. Mazingira wezeshi kwa ujumla wake katika ubunifu ni pamoja na kuwa na mfumo stahiki (ecosystem) inayosaidia wabunifu na bunifu nchini ,ikiwa ni pamoja na Kumbi za Ubunifu kuwapokea na kuwalea wabunifu, Sera na miongozo, mitaji.
0 Comments