Header Ads Widget

ACT WAZALENDO YAFICHUA UFISADI KATIKA MIRADI YA SERIKALI.


 Na Matukio Daima App, Zanzibar.

CHAMA cha ACT Wazalendo kimetangaza maeneo yanayokabiliwa na ufisadi ikiwemo miradi ya ujenzi wa barabara, uwanja wa amani na ukodishwaji wa bandari ya malindi visiwani Zanzibar.


Akihutubia Mamia ya Wafuasi na wanachama wa Chama huko Bubwini Mkoa wa Kaskazin Unguja Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama hicho Ismail Jussa amesema kuna dalili za kuwepo kwa ufisadi katika utekelezaji wa baadhi ya miradi.


Amesema kwamba serikali ya awamu ya nane imekuwa ikiidhinisha miradi ya ujenzi wa majengo ya umma na barabara bila ya kutangaza zabuni kinyume na sheria ya zabuni na ushindani iliyopitishwa na baraza la wawakilishi Zanzibar.


Akizungumzia kitendo cha mkandarasi wa kampuni ya ujenzi ya Orkun ya uturuki kupewa ulinzi wa usalama wa taifa na kutembea na kingora ni kwenda kinyume na utaratibu wa itifaki za matumizi ya huduma hiyo.


Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho juma duni haji, amesema Zanzibar imeshindwa kunufaika na rasilimali ya geni na madini licha ya kuwa mambo hayo yamo katika orodha ya mambo ya muungano .


Makamu mwenyekiti wa chama hicho ambae pia ni makamu wa kwanza wa rais Othman masoud amesema rais mstaafu dk salmin amour ndie aliekuwa wa kwanza kupinga vitalu vya mafuta Zanzibar kuchimbwa na kampuni moja kutoka Canada.


Chama cha ACT WAZALENDO kimekamilisha mikutano yake ya hadhara kwa awamu ya kwanza kwam ikutano 12 katika visiwa vya unguja na pemba ikiwa ni mikutano ya kwanza ya hadhara ya kisaisa kufanyika tangu kuruhusiwa na rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania dk samia suluhu Hassan baada ya kuzuwia kwa muda wa miaka saba chini ya uongozi wa marehemu dk Joseph Pombe Magufuli.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI