Header Ads Widget

CCM TANGA YATAKA MRADI WA VITUO VYA AFYA VYA KIRENGE NA MNYUZI UMALIZIKE HARAKA.



Na Mbaruku Yusuph-Matukio Daima APP, Korogwe.

CHAMA cha Mapinduzi mkoa wa Tanga kimemuagiza Mkuu wa Wilaya Korogwe kupitia Katibu Tawala wake kwamba ahakikishe vituo vya afya vya Kerenge na Mnyuzi vinamalizika haraka ili wananchi waweze kunufaika na huduma hiyo ya afya.


Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Tanga Rajabu Abdurahman alipokagua vituo hivyo wakati wa ziara yake Wilayani humo na kusema hajafurahishwa na utekelezaji wa miradi hiyo ambayo imeonekana kuchukua muda mrefu kumalizika.


Aidha aliiomba Ofisi hiyo ya DC kufuatilia kwa makini taarifa za kibank ili kuweza kujiridhisha uwepo wa fedha za miradi hiyo kama taarifa ya mkurugenzi inavyoeleza kuwa kipo kiasi cha fedha zimebakia baada ya matumizi ya mradi huo kuanza ingawa umesimama kwa sasa.


"Ninamashaka hizo fedha sijui kama zipo pamoja na madhaifu yaliyojitokeza kwa mkandarasi kama anadai na halipwi na kwanini asilipwe?'' Alihoji Rajabu.


Rajabu alisema Serikali imetoa pesa kwa ajili ya ujenzi wa vituo hivyo vya afya kwa lengo la kuwasaidia wananchi wanaoteseka kwa kutembea umbali mrefu zaidi ya km 40 kufuata huduma hiyo ya afya Korogwe Mjini jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya wananchi hao.


Alisema kinachofanywa na watendaji na Viongozi Wilayani hapo kwa kutokukamilisha ujenzi wa vituo hivyo ni kumchonganisha Rais,Mbunge na hata Diwani dhidi ya wananchi na kuonekana Serikali haiwajali wananchi wake.


Alisema vipo vituo vya afya vimejengwa kwa gharama hizo hizo za Shs Mil 400 karibu Mkoa mzima wa Tanga na majengo yote yamejengwa tofauti na Korogwe ambapo wamepokea shs Mil 500 kwa kituo kimoja na havijakamilika.


Aidha alisema pesa nyingi zimeelekezwa Wilayani Korogwe kwa ajili ya miradi ya vituo vya afya jambo la kusikitisha vituo hivyo havijakamilika na ni dalili za wazi zinazoonyesha Wilaya ya korogwe imeonyesha kiasi gani kuna uzembe wa usimamiaji wa miradi ya maendeleo.


Rajabu aliwataka viongozi waliopewa dhama na Rais wafanye kazi kwa weledi na watambue kufanya hivyo kutasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa kama sio kumaliza kero za wananchi hasa katika miradi ya kimaendeleo.


Hata hivyo alisema iwapo maagizo ya chama hayatatekelezwa basi watambue chama ni kikubwa kuliko mtu yeyote na Serikali ni kubwa kuliko nafasi mlizokuwa nazo na kama umepewa dhamana ni wajibu kuitumikia dhamana hiyo.


Kwa upande wake Mbunge wa Korogwe Vijijini Timotheo Mzava alisema kwanza wanamshukuru Mh,Rais kwa kutoa Bil 1 kwa ajili ya ujenzi wa vituo viwili vya afya ambapo Kituo cha afya cha Kerenge Shs Mil 500 na kile cha Mnyuzi Shs Mil 500


Aidha alisema changamoto ya utekekezaji wa miradi hiyo ni ucheleweshwaji na hata majengo yaliyokuwatayari hayakuanza kutumika ingawa uhitaji wa huduma hiyo ni kubwa kwa wananchi wa maeneo hayo.


Alitumia fursa hiyo kuiomba Serikali ijitoe kwa nguvu zote ili utekelezaji wa vituo hivyo vya afya vikamilike kwa wakati ili kuwaondolea adha wananchi hao kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya.


Akitoa taarifa fupi ya mradi huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Korogwe Halfan Magani alisema miradi hiyo imechelewa kutokana na taratibu za kimanunuzi kupitia mfumo wa force Account kupitia kamati ambazo zipo Kijijini.


Aidha alisema mbali ya changamoto hiyo ya mfumo wa kimanunuzi pia  mkandarasi alishindwa kuendelea na mradi Halmashauri ipo kwenye mchakato wa kumtafuta mkandarasi mwengine ili aweze kumalia sehemu iliyobaki.


Kaimu mhandisi wa Wilaya Eng,Mungi alisema baada ya maelekezo hayo wanatarajia ndani ya miezi 2 miradi itakuwa hiyo itakuwa imemalizika na matarajio hadi mwezi wa kumi mwaka.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI