Header Ads Widget

WANANCHI RUTORO WATAKIWA KUHIFADHI MAENEO KIMKAKATI KWA AJILI YA UWEKEZAJI WA MALIASILI

  


Wananchi wa Kijiji cha Rutoro Wilayani Muleba Mkoani Kagera wanaoishi kwenye Ranchi ya Kagoma wametakiwa kuhifadhi na kutenga maeneo  kwa ajili ya uwekezaji katika Sekta ya Maliasili na Utalii baada ya kumilikishwa ardhi.


Ameyasema hayo jana katika ziara ya Mawaziri wa Kisekta iliyolenga kutatua mgogoro  wa Ranchi  ya Kagoma Mkoani Kagera.


Amefafanua kuwa endapo wananchi watayatunza vizuri maeneo watakayopangiwa wataweza kuanzisha miradi ya Upandaji Miti, ufugaji nyuki na shughuli nyingine zitakazowasaidia kukuza uchumi wao.


"Ujumbe wetu ni kuhakikisha kwamba yale maeneo ambayo tutayahifadhi vizuri tutayatunza vizuri tuyafanye kuwa rasilimali za kesho kwa maendeleo ya  kizazi cha sasa na baadae" Mhe. Masanja amesisitiza.



Aidha, amewaasa wananchi hao kuacha tabia ya  kuvamia maeneo na badala yake wawe na mpango mzuri wa matumizi bora ya ardhi.


"Maisha ya kutangatanga  yamepitwa na wakati mnatakiwa muwe na maeneo ya kuyahifadhi  kwa ajili ya kuwapatia vipato na mengine yatakuwa kwa ajili ya shughuli za kibinadamu " Mhe. Masanja amesema.


Kamati ya Mawaziri wa Kisekta imeridhia Halmashauri ya Wilaya ya Muleba  kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi pamoja na kuwagawia wananchi maeneo mengine yaliyopangwa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI