Na Chausiku Said-Matukio Daima, Mwanza.
Jumla ya wafanya biashara 850 kutoka Tanzania na Nje ya Tanzania wanatarajia kushiriki katika maonesho ya Biashara ya Afrika mashariki huku washiriki 420 kutoka sekta mbalimbali wamethibitisha kushiriki katika maonesho hayo na wafanya biashara wadogo wadogo 210 .
Hayo yamelezwa na mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara viwanda na kilimo Mkoa wa Mwanza (TCCIA) Gabriel Mugini alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari na kueleza kuwa maonesho ya 18 yanatarjia kuanza Agosti 25 Hadi Septemba 3 katika viwanja vya Furahisha Wilayani Ilemela Mkoani hapa.
Huku maonesho ya 17 ya mwaka Jana walifanikiwa kupata jumla ya washiriki 320 kati ya 450 kutoka katika mataifa 11 ambayo ni pamoja na Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Sudani kusini, Malawi, Nigeria, Singapore, India, China pamoja na Tanzania wakiwa wenyeji.
Mugini Amesema kuwa lengo la Maonesho hayo Kwa wafanyabiashara na Serikali ya Mkoa na Taifa ni kuwakutanisha wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima kufahamiana na kufungua fursa za masoko Kwa bidhaa zao na kitengeneza mtandao wa kibiashara kati ya wafanyabiashara wa Tanzania, Afrika Mashariki na nje ya Bara la Afrika.
Aidha ameeleza kuwa maonesho hayo yame na manufaa mbalimbali Kwa wananchi na wafanyabiashara na Taasisi za umma mbalimbali Ndani na Nje ya Nchi Kwa wajasiliamali wadogo, wakati na wakubwa kuonesha bidhaa zao Kwa wigo mpana Kwa wananchi walioudhulia maonesho hayo.
Taasisi za kifedha kuongeza wigo wa kutoa huduma zao na mzunguko wa kifedha pamoja na kutoa Elimu Kwa uuma kutokana na huduma zao, pamoja na mzunguko wa kifedha kuongezeka ndani ya Mkoa kutokana na ujio eawageni mbalimbali wanaoshiriki maonesho hayo.
Kwa upande mwingine ametoa wito Kwa wafanyabiashara wa Kanda ya ziwa na wananchi Kwa ujumla kutembelea maonesho hayo ili waweze kujifunza na kujipatia bidhaa mbalimbali.
Katika maonesho hayo ya 18 Afrika mashariki mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa viwanda na Baishara Ashatu kijaji huku kauli mbiu ikiwa "Mazingira bora ya Biashara ni kivutio Cha kukuza uwekezaji wa biashara viwanda na kilimo Tanzania, Afrika mashariki na Afrika".
0 Comments