Na Gift Mongi MATUKIODAIMA APP
Moshi
Wakala wa vipimo (WMA)mkoa wa Kilimanjaro kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 walifanikiwa kuwatembelea wafanyabiashara 9824 katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo lengo likiwa ni kujiridhisha na uhalali wa vipimo vinavyotumika.
Katika idadi hiyo jumla ya vipimo 22657 viliweza kuhakikiwa ambapo 3470 kati yake vilikutwanna dosari na viliweza kurekebisha na kuruhisiwa kuendelea na matumizi ya kibiashara kama kawaida.
Salum Masinde ni meneja wa wakala wa vipimo mkoa wa Kilimanjaro ambapo alisema pia kati ya vipimo hivyo vingine 312 vilishindikana kurekebishwa hivyo vikaondolewa katika matumizi.
Alisema katika kipindi hicho waliweza kutembelea wauzaji wa gesi,maeneo ya pampu za mafuta lakini pia katika maeneo ya mizani lengo likiwa ni kuangalia utiifu wa sheria.
'Tulifanikiwa kutembelea sehemu zote ambazo zinatuhusu kuangalia utiifu wa sheria na kama Kuna uvunjifu ama laa maana ni lazima vipimo vihakikiwe na kama unavyojua tupo katika sehemu mbalimbali'amesema
Alisema pia katika sekta ya gesi walifanikiwa kukaa na wauzaji wa nishati hiyo na kuendelea kuwakumbusha umuhimu wa kuwa na mizani ili mteja aweze kujiridhisha na ujazo anaonunua kama umelingana na kile kilichoandikwa .
'Pia tumehakiki dira za maji na tumekutana na mamlaka za watoa huduma za maji na kuhakikisha dira hizo kabla ya kumfikishia mteja ili kuondoa malalamiko toka pande zote mbili kati ya mtoa huduma na mteja mwenyewe'alisema
Alisema jumla ya dira za maji elf 13 zilihakikiwa lakini pia ni zoezi endelevu kwa mwaka huu lengo ni kuhakikisha kila mteja anayefungiwa dira mpya ya maji inakuwa imehakikiwa na wakala huyo.
Kadhalika aliongeza kuwa katika vituo vya mafuta mkoani Kilimanjaro asilimia 70 walikagua pampu zake kwa njia ya kushtukiza ambapo kati yake pampu mbili pekee ndizi zilizoonekana zina dosari na kufanyiwa marekebisho.
'Sheria kama inavyoelekeza vipimo ni kila baada ya miezi 12 lazima vihakikiwe ndio tunataka utekelezaji wake na mwaka huu ni lazima tupite katika maeneo yote ya ukaguzi na mwezi huu tunaanzia ukaguzi katika wilaya ya Same hivyo wafanyabiashara wajitokeze kuhakiki vipimo vyao'alisema
Sadick Kamugisha mkazi wa Bomang'ombe wilayani Hai alisema uhakiki wa mizani japo upo kisheria ila una manufaa kwa mfanyabaishara na mteja mwenyewe maana kama mizani itakuwa na hitilafu mojawapo atapunjwa.
'Tatizo watu wanafanya kimazoea tu ila ukweli ni kuwa hili zoezi lina faida kubwa sana kwa pande zote mbili kati ya muuzaji na mnunuzi'alisema Kamugisha
Mwisho
0 Comments