Na Gift Mongi MATUKIODAIMA APP MOSHI.
VIJANA wa chama cha mapinduzi(UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini kwa pamoja hivi sasa wamekuja na maono ya kipekee katika kuungana na mwenyekiti wa chama hicho taifa Dkt Samia Suluhu Hassan katika kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo hapa nchini.
Ikiwa ni takribani mwaka mmoja sasa kupita tangu kuzinduliwa kwa filamu ya Tanzania the royal tour wadau mbali mbali wamejitokeza kuunga mkono jitihada hizo ambazo zimeonyesha kuzaa matunda.
Hivi sasa kundi la vijana wapatao 100 wilaya ya Moshi Vijijini wamehamasika kuvitangaza vivutio hivyo hususan vile vinavyopatikana katika wilaya ya Moshi Vijijini ambapo pia baadaye huenda ikawa katika maeneo mengine.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi mwenyekiti wa umoja huo Yuvenail Shirima amesema kuwa mara baada ya kumaliza kikao cha baraza hapo julai 15.2023 wajumbe wataenda kutembelea vivutio mbali mbali vilivyopo wilaya ya Moshi Vijijini.
'Tunaenda kumuunga mkono rais wetu katika kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii na hivyo tukimaliza kikao cha baraza tutaenda kutembelea vivutio vilivyopo wilaya ya Moshi Vijijini ikiwemo eneo la Kinukamori'alisema
Alisema jitihada hizo pia zitaenda kugusa katika maeneo mbali mbali ya utalii kama maporomoko ya Marangu na sehemu nyingine na huenda ikawa hata nje ya mkoa na hii ni matokeo ya kuunga mkono filamu ya 'The royal TOUR'.
Mwanaima Said ambaye ni mkazi wa Moshi amesema jitihada zinazofanywa na vijana hao ni vyema zikaungwa mkono na makundi mengine katika jamii ili kukuza sekta ya utalii.
'Hawa vijana wamekuja na mawazo mazuri katika kuhamasisha utalii na itapendeza kama makundi mengine kwenye jamii yataenda kuiga kutoka kwao maana Kuna manufaa'"_alisema
0 Comments