Maafisa wa Marekani na Urusi watakutana katika jimbo la Alaska kabla ya mkutano wa Ijumaa unaotarajiwa kati ya Rais Donald Trump na Vladimir Putin.
Wawili hao watakutana kwa mara ya kwanza baada ya miaka sita, huku Trump akijaribu kutunga ahadi muhimu ya kampeni ya kumaliza vita vya Urusi nchini Ukraine.
Rais wa Marekani, ambaye amejionyesha kama mtu wa kuleta amani duniani, anatumaini kuimarisha uhusiano wake wa kibinafsi na Putin ili kufikia muafaka wa kusitisha mapigano ambapo wengine wameshindwa.
Siku ya Alhamisi alikadiria kuwa kwa "fursa ya 25%" mkutano huo hautafanikiwa.
Kiongozi wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameondolewa kwenye mazungumzo hayo, na kuonya kuwa maazimio yoyote yatakayotolewa bila kuwepo kwake hayatakuwa na maana yoyote.
Huko Anchorage kuna dalili chache za mkutano wa hali ya juu unaokuja, isipokuwa vyombo vya habari vya kimataifa ambavyo vimefika kwenye eneo hilo.
Mkutano wa Ijumaa kati ya viongozi hao wawili utafanyika katika kambi ya kijeshi ya Marekani iliyo karibu - ikiwa ni taswira ya wasiwasi wa kiusalama na mpango wa kuketi kwa ajili ya mazungumzo hayo umefupishwa, ikipagwa kuwa mkutano huoutadumu kwa saa chache tu.
Mkutano huo unakuja wiki moja baada ya makataa ya Trump yakikaribia kwa Urusi kufikia usitishaji vita au kukabiliwa na vikwazo vipya vikali.






0 Comments