Header Ads Widget

SHIRIKA LA HHU LAZIJENGEA UWEZO KAMATI ZA AFYA KIFANYA NJOMBE

Mratibu wa jitihada za jamii Halmashauri ya mji wa Njombe Daniel Mwasongwe
Afisa miradi wa Shirika la HHU bwana Calvin Mwinuka


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Ili kuboresha utoaji wa huduma za afya kwenye Zahanati na vituo vya afya kwenye vijiji na kata kamati za usimamizi za afya kwenye zahanati na vituo vya afya zimetakiwa kutambua wajibu wao  badala ya kuwaachia wataalam wa Afya pekee.


Akitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati hizo chini ya shirika la Highlands Hope Umbrela HHU Mratibu wa jitihada za jamii toka halmashauri ya mji wa Njombe bwana Daniel Mwasongwe amewataka wajumbe hao kutoka vijiji vya Lilombwi,Kifanya na Liwengi kata ya Kifanya kwenda kutekeleza wajibu wao kwa kadri ya miongozo badala ya kukaa kimya na kusubiri mambo yaharibike kwenye zahanati na vituo vyao vya afya.


Kwa niaba ya Mkurugenzi wa HHU Afisa mawasiliano bwana Robert Shejamabu na Calvin Mwinuka afisa miradi wa shirika hilo wamewataka wajumbe wa kamati hizo kutambua kuwa nafasi walizonazo katika kuihudumia jamii ni kubwa na hivyo wanaowajibu wa kutoa matokeo chanya.


Kwa upande wao wajumbe wa kamati hizo akiwemo Coretha Mkole,Ditrick Danda,Atilio Peter na Sarah Chombe wamekiri kupokea mafunzo hayo na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi kwa kuwa baadhi yao walikuwa hawafahamu baadhi ya majukumu wanayopaswa kutekeleza.


Shirika la HHU Limekuwa likitekeleza miradi mbalimbali ya Afya,Utawala bora pamoja na Kilimo.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI