Header Ads Widget

RAIS SAMIA :DHAMIRA YA SERIKALI NI KUWA NA JKT IMARA

 


NA HAMIDA RAMADHAN MATUKIO DAIMA APP DODOMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Serikali ni kuiboresha JKT ili liwe Jeshi la kisasa zaidi linaloendana na wakati na kutimiza majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu .


Pia amesisitiza mafunzo yanayotolewa na JKT yawasaidie vijana kuwa wazalendo wa kweli wanaothamini utaifa, umoja na mshikamano wa Watanzania na wanaopenda kufanya kazi kwa moyo wa kujituma na kujitolea.


Rais Samia ameyasema hayo leo jijini hapa kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT.


"Kwa vijana watakaoendelea na kazi katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama baada ya mafunzo yao, nataka wawe na weledi wa kuaminika, kutumainiwa na wanaoweza kweli kuilinda na kuitetea nchi yao bila hofu,"


Na kuongeza" JKT ilianzishwa rasmi Julai 10, 1963, ambapo hatua hii ilikuwa ni utekelezaji wa azimio la kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Aprili 19, 1963 chini ya uongozi wa Rais wa Awamu ya Kwanza, Hayati Mwl. Julius Nyerere," amesema .


Amesema Kutokana na umuhimu wa JKT katika kuwaandaa vijana, mwaka 1964 wakati akihutubia vijana wa JKT kwenye Kambi ya Mgulani, Hayati Mwl Nyerere alisisitiza kuwa JKT liwe lango kuu ambalo kila kijana atalazimika kulipita kabla ya kwenda kulitumikia taifa katika nafasi mbalimbali, huku ndiko tunakotaka kuelekea,"alisema.


Amesema mwaka huu, idadi ya vijana waliomaliza chuo na kuingia JKT kwa ajili ya mafunzo imeongezeka,na kueleza matumaini ya Serikali kwamba kila mwaka idadi hiyo itaendelea kuongezeka mbali ya wale vijana wanaojitolea kwa hiari.


Alifafanua kuwa kwa miaka 60 ya uwepo wa JKT, wamekuwa wakitekeleza dhima ya msingi ya kuwajengea vijana wetu utayari wa kulitumikia taifa lao kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa kujenga umoja, uzalendo, nidhamu na uadilifu miongoni mwa vijana, sifa ambazo ni za msingi kwa vijana ili waweze kutoa mchango 


Alisema ndani ya JKT limekuwa na mafanikio mengi ikiwemo kutoa ujuzi na mafunzo mbalimbali kwa vijana ikiwa ni pamoja na kazi za mikono ambazo zinawafungua sana vijana kuingia kwenye maeneo mengine ya kazi na kuweza kujitegemea.


"Yote yanayofanywa na JKT ni utekelezaji wa Dira ya Taifa ambapo kwa sasa tunatekeleza dira ya mwaka 2025 yenye kusisitiza katika kujenga uzalendo, utaifa na kuimarisha umoja,"amesema


"JKT pia inatekeleza Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano unaotekelezwa nchini kwa kuwa Mpango huo umesisitiza kuchagiza wajibu wetu wa kutumia rasilimali za ndani ili kujitosheleza na matakwa yetu ya ndani ya nchi ili kuondoa utegemezi bila kusahau mila na desturi zetu,"alisisitiza.


Pamoja na hayo aliongeza kuwa ,"azma ya Serikali ni kuongeza uwezo kwa JKT ili iendeshe majukumu yake na waweze kulea vizuri vijana wetu, ninafarijika kuona muitikio wa vijana kujiunga na Jeshi hili umekuwa mkubwa,programu ya "Buiding Better Tomorrow" ni lengo la Serikali kuunganisha/kuratibu shughuli zinazotekelezwa na JKT kuingia kwenye mpango huu ili vijana wawe na mwelekeo mzuri,",alisisitiza.


ameshiriki sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT)huku akiielekeza Wizara ya Ulinzi na JKT kuandaa mpango mkakati wa kurekebisha makambi kwenye Jeshi la JKT katika upande wa malezi ya vijana.


Akizungumza Jana jijini hapa kwenye maadhimisho hayo Rais Samia ameitaka pia Wizara hiyo, kuliwezesha Shirika la SUMA JKT kupata mikopo ili wazalishe na waweze kurejesha mikopo na shirika liweze kuendelea, na kwamba kama ikitakiwa udhamini wa Serikali itakuwa tayari.


Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa alisema mafunzo ya JKT ni sehemu muhimu ya mchango wa amani iliyopo nchini na kwamba Wizara itaendelea kushirikiana na wizara za kisekta kuboresha mafunzo stadi za kazi kwa vijana wa JKT na kuwawezesha kuwapatia ujuzi na maarifa zaidi ya ilivyo sasa ili baada ya kuhitimu mafunzo hayo waweze kujitegemea na kuanzisha shughuli mbalimbali za ujasiriamali bila kusahau maendeleo ya michezo na sanaa.


Alisema ili kutekeleza maelekezo ya Rais Samia Wizara yake itashirikiana na sekta za kilimo, mifugo na uchumi wa buluu pamoja na kufungamanisha sekta hizi na sekta ya viwanda ili kuimarisha JKT na JKU kuwa vyombo vya kuwapatia vijana ujuzi wa kujiajiri na kuajiriwa, pia kuwa vyombo mahiri vya huduma za uzalishaji mali.


"Dhumuni kuu la kusanyiko hili ni  kikubwa kubadilisha fikra za kikoloni kwa vijana waliohudhuria mafunzo yake, JKT imefanikiwa kuwajenga vijana katika hali ya umoja, moyo wa kupenda kazi, uadilifu, nidhamu, uelewano bila kubaguana kwa misingi ya ukabila, dini, jinsia hivyo kudumisha uhuru na amani ya Taifa letu,"alisema 



Alieleza kuwa JKT imefanikiwa kuwa na ongezeko la idadi ya vijana wanaopata mafunzo ya Jeshi hili ambapo mwanzo lilianza na vijana 11 lakini kwa sasa vijana waliopo makambini wanaohudhuria mafunzo kwa mujibu wa Sheria ni 52,000.


Pamoja na hayo alisema Uanzishwaji wa vikosi, kambi mpya za JKT na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya vikosi, umesaidia kuongeza idadi ya vijana wanaoshiriki mafunzo ya JKT. JKT imekuwa ni chombo muhimu cha muwajenga vijana na kukuza uzalendo


"JKT inaendelea kuaminika na kufanya miradi muhimu ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa Ikulu ya Chamwino pamoja na majengo na miradi mingine ya Serikali,katika kuhakikisha Jeshi linajitegemea kwa chakula na kuwepo kwa usalama wa chakula nchini, JKT ilianzisha skimu ya umwagiliaji katika shamba la mpunga  ambayo inaendelea kujengwa,"alisisitiza


Kwa upande wa SUMA JKT alieleza kuwa inatekeleza kazi zake mbalimbali za ujenzi, kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda na biashara. Shirika limefanikiwa kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake kwa kuendelea kuchangia gharama za mafunzo ya vijana na kuchangia katika Pato la Taifa kwa kutoa gawio na kulipa kodi stahiki kwa Serikali. 


Akitoa taarifa ya JKT Meja jenerali Rajabu Mabele alisema Jeshi hilo Lina majukumu ya uzalishaji mali na ulinzi wa Vijana.


Alisema Jeshi la Kujenga Taifa limefanya kazi kubwa na nzuri ya kujenga moyo wa utaifa na uzalendo miongoni mwa vijana waliopitia katika Jeshi hilo. Hapa ni mahali ambapo vijana wa itikadi zote, rangi zote, makabila yote, dini zote hukutana, kuishi pamoja na kufanya mafunzo na kazi kama ndugu wa familia moja.


"JKT limekuwa mfano wa malezi ya vijana  pengine hata ile tabia ya Watanzania wengi kutoulizana mabila imetokana na kuwa na vijana wazalendo wa wanaopitia JKT,huwa wanakutana na vijana mbalimbali kutoka kila kona ya nchi yetu, ndiyo maana hawana muda hata wa kuulizana makabila kwa vile wote hujiona ni wamoja,"alisemaa


Alisema majukumu ya msingi ya JKT ni malezi ya vijana, uzalishaji mali na ulinzi wa Taifa, tangu kuanzishwa kwake rasmi Julai 10, 1963, hadi sasa Jeshi hili linatekeleza majukumu yake kwa ufanisi.


"JKT imefanikiwa kuwa na ongezeko la idadi ya vijana wanaopata mafunzo ya Jeshi hili ambapo mwanzo lilianza na vijana 11 lakini kwa sasa vijana waliopo makambini wanaohudhuria mafunzo kwa mujibu wa Sheria ni 52,000,"alisema 


Alisema Uanzishwaji wa vikosi, kambi mpya za JKT na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya vikosi, umesaidia kuongeza idadi ya vijana wanaoshiriki mafunzo ya JKT. JKT imekuwa ni chombo muhimu cha muwajenga vijana na kukuza uzalendo


Pamoja na hayo alisema JKT inaendelea kuaminika na kufanya miradi muhimu ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa Ikulu ya Chamwino pamoja na majengo na miradi mingine ya Serikali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI