NA THABIT MADAI,ZANZIBAR -MATUKIO DAIMA APP
MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli Tanzania (PURA) imesema kuwa, imefanikiwa kuchimba Visima 96 vya Mafuta na kwamba kati ya hivyo, 44 vimegundulika kuwa na gesi asilia.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Mkutano wa KImataifa wa Sekta ya Nishati na Viwanda, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli Tanzania (PURA) Charles Sangweni amesema kuwa, Visima hivyo vingi vipo katika bahari.
"Katika Visima 96 tumepata Gesi Visima 44 na vingi vipo katika Bahari Kuu, Tunaamini kwamba bado muda na uwezo wa kuendelea kutafuta," amesema.
Aidha ameeleza kuwa Tanzania maeneo ambayo yanaviashiria yanafika Squer Kilimita 534,000 ambayo karibu asilimia 50 ya Ukubwa wa Nchi.
"Nataka niwaambie kuwa katika hizi Squere Kilimita 534,000 tumeweza kufanya utafita na kuchimba Squer Kilimita 160,200 tu sawa na asilimia 30 tu ambapo tunakazi kubwa ya kuhakikisha hizi Asilimia 70 tunazifanyia kazi ukizingatia tupo katika kipindi cha mpito cha kutumia Nishati Jadidifu," ameeleza.
Amebainisha kuwa, Uwepo wa Mafuta Nchini ni mkubwa ukilinganisha na Maeneo mengine barani Afrika.
Hata Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa PURA ipo katika hatua ya kuandaa Mkataba kifani ambao watautumia kwenye Mnada wa kitalu wanaotarajia kuufanya mwishoni mwaka 2024.
0 Comments