Header Ads Widget

ONGEZEKO LA WANANCHI DODOMA YAPEKEKEA MJI KUKUA KIHOLELA BILA MPANGILIO

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema  jiji la Dodoma limekuwa na ongezeko la wananchi hali inayopelekea matumizi ya ardhi kuwa ni mengi na mengine kuwa ya kiholela bila mpangilio 


Ili kutatua changamoto hiyo mkoa wa Dodoma kupitia Mkuu wa mkoa wa Dodoma imeandaa timu kwa ajili ya kutatua na kumaliza migogoro kabisa.


Senyamule ameyasema jijini Dodoma wakati akizindua mpango mkakati kwa ajili ya kushughulikia na kutatua migogoro ya ardhi kwa jiji la Dodoma.


"Kuna changamoto mbalimbali zinazochangia migogoro hii kushindwa kuisha kutokana na uchache wa vifaa vya tehama, ukosefu wa huduma bora kwa wananchi,eneo la jiji kuwa dogo, lugha mbaya kwa wananchi zinazotolewa na watumishi wa jiji,kipandikizi yaani kupandikiza zaidi ya kiwanja kimoja kupewa watu tofauti pamoja na wananchi kupuuza jumbe za simu" Amesisitiza Senyamule.


Na kuongeza Kusema"Niwaombe wananchi  na wakazi wa mkoa wa  Dodoma kuacha kudanganya maeneo ya makazi ili kuepusha migogoro ya ardhi," amesema


Amesema  jambo Hilo litafanyika ndani ya miezi 6 kuanzia Julai hadi Disemba ambapo kutafanyika uhakiki wa maeneo ambayo yanamalalamiko .


"Wahusika wanavamia maeneo ambayo sio ya kwao pamoja na kurekebisha mifumo kwa kushirikiana na ofisi ya Rais tamisemi," amesema


Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri amesema kuwa mpango huo utaweza kuwasaidia kutambua mapungufu gani ya ndani na madhaifu gani ya nje ili kuishi matarajio ya kiongozi wa kitaifa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuhakikisha jiji la Dodoma linapagwa vizuri ili kuendana na hadhi ya makao makuu ya nchi.


" Ni matumaini yake kwamba elimu ya kutosha itatolewa kwa kamati ili kuhakikisha wanakuwa na uelewa huku akisisitiza maeneo ya wazi kupewa watu sahihi ili kuhakikisha wanajenga vitu vyenye manufaa kwa wananchi,"


Na kuongeza"Mifugo kuzurura mjini nilipata nafasi ya kuongea na wafugaji tulikuwa na kikao kizuri hivyo ni rai yangu tuliyokuwa tukiyaongelea yatakuwa yamezingatiwa,wakati mmoja tulikamata mifugo ya kiongozi mmoja,akanipigia simu nikamwambia lazima ulipe fidia haijalishi wewe ni nani huwezi acha mifugo kiholela" Amesema Shekimweri.


Aidha ametoa rai kwa watumishi wa ardhi kuhudumia wateja vizuri kwa kutoa kauli nzuri kwa wateja pamoja na kuheshimu watu.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI