Header Ads Widget

TUNAZITAKA KAMPUNI ZA BIMA KUTOA MASLAHI SITAIKI KWA WATEJA WAO, TOYOTA.

 


NA CHAUSIKU SAID MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.


Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imezitaka kampuni za Bima kuhakikisha wanatoa maslahi stahiki Kwa wateja Kwa kisimamia na kushughulikia malalamiko yao.


Hayo yamebainishwa na Meneja wa Mamlaka ya Bima Kanda ya ziwa Richard Toyota ameeleza kuwa ni wajibu wa kampuni kuhakikisha inatimiza wa mkataba wake Kwa kutoa kipaumbele Kwa wateja wao.


Toyota Amesema kuwa ni wajibu wa kampuni na watoa huduma  kuhakikisha wanaweka maslahi ya wateja wao ili kuwezesha huduma za hizo kuwa bora na zenye mvuto Kwa wanatimiza wajibu wa mkataba wao.


"Kwa hiyo kitendo Cha makapuni hayo kutotoa haki kwa wakati ni Changamoto kubwa na sisi ndio wasimamizi wa wananchi "Alisema Toyota.


Aidha amefafanua kuwa pindi tukio lolote la linapotokea na kusababisha hasara mkata bima anatkiwa kutoa taarifa ya janga hilo ndani ya masala 48 Kwa mdomo na maadishi ndani ya siku 7.


"Mkata bima anapotoa taarifa lazima aeleze jinsi tukio lilivuokuwa ili kampuni ya bima iwajibike baada ya kupokea taarifa ndani ya masaa 48 Kwa kumpa nyaraka zinazostahili kuwasilishwa ili kuanza Kwa mchakato wa madai kuanza" Alisema Toyota.


 Toyota amesema kuwa Kwa mjibu wa sheria ya bima Na. 10 ya mwaka 2009 kampuni ya bima inapaswa kushughulikia madai ya wateja mfupi kulingana na ukubwa wa janga na uthibitisho kuwa halali.


Hata hivyo ameeleza kuwa baada ya kampuni hiyo kujiridhisha kuwa janga hilo ni sahihi na kutoa hati ya kukubali kampuni hiyo itawajibika kutoa fidia Kwa mteja ndani ya siku 45.


Kwa upande mwingine Meneja huyo ameeleza kuwa takribani matukio 5 hadi 10 Kwa mwezi wateja hutoa malalamiko juu ya kucheleweshwa huduma kutoka kampuni mbalimbali za bima pamoja na kutopata stahiki zao,

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI