Header Ads Widget

RC KHERI AWAFUNDA WATUMISHI MANISPAA YA IRINGA ,ATAKA KUTOA TAARIFA ZA VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WA AMANI

 


NA MATUKIO DAIMA MEDIA ,IRINGA

SERIKALI ya mkoa wa Iringa imewataka watumishi wa umma katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kujenga utamaduni wa kutoa taarifa wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa amani katikw maeneo yao.

Alisema kuwa jukumu la serikali kuepusha jamii kipata matatizo na sio kwenda kuwafariji baada ya tatizo kutokea.


Akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa leo wakati wa kikao chake cha kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa .

Kheri alisema ni jukumu la watumishi wa umma kuwa watu wa kwanza kujua viashiria hivyo vya uvunjifu wa amani kwenye maeneo yao.

Pia alitaka ajenda ya usafi katika Mji kuwa kipaumbele kwa Halmashauri hiyo kuwapanga wafanyabiashara katika maeneo rasmi na sio kuacha biashara kufanywa holela.

Alisema Mji wa Iriinga umekuwa na sifa kubwa ya usafi hivyo lazima sifa hiyo kuendelea kudumishwa.

"Niombe katika hili kuwapongeza Sana Manispaa ya Iringa huyu mkandarasi mliyempata anafanya kazi kubwa sana ya usafi mmepata mkandarasi sahihi sana anafanya kazi nzuri "

Alisema kwenye suala la usafi Manispaa ya Iringa inafanya vizuri mfano Gadeni ya IRUWASA ila kwa sasa imesimama kama suti ya kuazima hivyo lazima kuendelea na maeneo mengine.

Mkuu huyo wa mkoa aliagiza Halmashauri kuweka mpango wa kupanda maua katika maeneo mbali mbali ili mji kuwa na mwonekano mzuri.

Aidha alitaka suala la usafi wa mji kwenda sambamba na mipango miji na suala la masta Plani kupewa nafasi badala ya watu kupenyeza pesa .

Hivyo kuagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) kufuatilia ujenzi holela unaoendelea ndani ya Manispaa ya Iringa .

"Watendaji wamekuwa wakiwajibika kuzuia ujenzi holela ila wapo baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumia vibaya nafasi zao kwa kuruhusu ujenzi kuendelea.

Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa alitaka suala la usafi lipewe nafasi kwa mtu mmoja mmoja kwa kuhakikisha eneo lake la kazi ama analoishi linakuwa safi.

Alisema katika suala la usafi kwenye majengo binafsi anapongeza Tanesco ,IRUWASA na TRA kwa kuwa na ofisi zenye mvuto kwa kupaka rangi pindi inapohitajika .

"Lazima majengo ya serikali yapendeze kwa kutokuwa na nyasi kupaka rangi inapohitajika sio huduma nzuri ofisi chafu  kuna wengine kwenye ofisi zao picha zipo toka za TANU walizoweka babu zetu lazima tuweke mazingira bora usafi unaongeza thamani ya mji pia"

Aidha aliagiza Manispaa kuendelea kufuatilia changamoto mbali mbali zinazohusu wananchi kwa kuwafikia kila wakati ili kutoa maoni na kero zao.

kuwa iwapo watumishi wa umma hawatapata nafasi ya kwenda kusikiliza wananchi kutakuwa na shida ya utekelezaji wa mipango mbali mbali  inayotolewa pesa na serikali.

Wakati huo huo mkuu huyo wa mkoa ameagiza Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kutumia fedha za miradi zinazoletwa kutekeleza miradi yenye ubora na si vinginevyo.

Alisema Manispaa ya Iringa kuna miradi iliyokamilika vizuri na ipo miradi iliyopo hatua nzuri na ipo miradi inayosuasua hivyo lazima miradi hiyo kukamilika bila kusahau kutoa taarifa kwa wananchi mradi unapoanza na unapomalizika kwenda kimya kimya bila wananchi kujua.

"Fedha za serikali zinapokuja lazima uwazi uwepo hakuna siri kwenye fedha za serikali maana serikali inaleta pesa kwa ajili ya wananchi hivyo ili waweze kushiriki katika miradi hiyo lazima wajulishwe"

Alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa serikali kuu imeleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa barabara ya mchepuko ya Iringa ,ujenzi wa soko la Kihesa  ,vituo vya afya ,elimu na miradi mingine mingi.

Hata hivyo alisema ili miradi kuendelea kukamilika ni lazima Manispaa ya Iringa kuongeza nguvu katika usimamizi wa miradi na kutimiza malengo ya kukusanya kiasi cha Tsh bilioni 8 iliyokusudiwa.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI