Header Ads Widget

SERIKALI KUANGALIA UWEZEKANO WA KUWA NA TOZO ZINAZOFANANA KWENYE MAENEO YA MIGODI YA MADINI

 


SERIKALI imesema inaangalia uwezekano wa kuwa na tozo zinazofanana kwenye maeneo ya uchimbaji madini kuepuka kila eneo kuwa na tozo tofauti ili kuwapunguzia kero wachimbaji nchini. 


Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Dk Dotto Biteko wakati alipofanya ziara kwenye  majangwa ya uzalishaji chumvi kwenye kampuni za Sea Salt Kijiji cha Saadani na HJ Stanley anda Sons Kijiji cha Kitame Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.


Aidha amesema kuwa serikali imeondoa tozo 17 kwa wazalishaji wa chumvi ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa hiyo kwenye soko la ndani na nje ya nchi.


Amesema kwa sasa Halmashauri kila moja inatoa tozo tofauti na nyingine hali ambayo inasababisha mkangannyiko ambapo lengo la serikali ni kuongeza uzalishaji.


"Tunataka uzalishaji wa chumvi nchini uongezeke na ziada iuzwe nje ya nchi ili kuongeza mapato pia kutoa ajira kwa wananchi kwenye maeneo ya uzalishaji,"alisema Biteko.


Ofisa Madini Mkoa wa Pwani Mhandisi Ally Maganga alisema kuwa Wilaya ya Bagamoyo inazalisha chumvi tani 90,000 hadi 100,000 kwa mwaka na kuingiza kati ya shilingi milioni 300 hadi milioni 350.


Mkurugenzi wa kampuni ya H J Stanley and Sons Richard Stanley alisema kuwa baadhi ya changamoto ni kukosekana kwa umeme, maji na ubovu wa barabara.


Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Shauri Selenda alisema kuwa kilio cha wawekezaji hao kinafanyiwa kazi kwa kuboresha miundombinu na upatikanaji wa maji na umeme na barabara.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI