Header Ads Widget

MBUNGE ZUENA AWATAKA WANANCHI KATA YA NJORO KUMCHAGUA MGOMBEA UDIWANI KUTOKA CCM.



NA WILLIUM PAUL, SAME.

WANANCHI wa kata ya Njoro wilayani Same mkoani wametakiwa kutofanya makosa katika marudio ya uchaguzi mdogo wa kata hiyo utakaofanyika Julai 13 mwaka huu na kuombwa kumchagua mgombea anayetokana na Chama cha Mapinduzi, Omari Abdallah.


Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri wakati wa vikao vya tathimini za kampeni vilivyofanyika katika matawi ya Njoro na Ishinde ambapo alikutana na viongozi wa Chama ngazi za matawi na kata pamoja wanachama wa CCM kata.



Alisema kuwa, chama cha Mapinduzi kimewaletea mgombea sahihi ambaye atawatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo na kuendana na kasi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani.


"Wananchi mnawajibu wa kuhakikisha mnachagua mgombea anayetoka na CCM katika uchaguzi huu wa marudio ili kukamilisha mafiga matatu na kunufaika na chama chenu chenye nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo" alisema Mbunge Zuena.



Aidha Mbunge huyo alisema, Ilani inayotekelezwa kwa sasa ni ya Chama cha Mapinduzi na kuwataka kumchagua Omari Abdallah ili aweze kuisimamia Ilani hiyo kwa vitendo.


Alisema kuwa, jukumu la chama cha Mapinduzi ni kuleta maendeleo na kuwataka kukikopesha imani chama hicho kwa kumchagua mgombea wake nacho kitawalipa maendeleo.



Katika hatua nyingine Mbunge huyo aliwataka wakinamama kuhakikisha wanawahimiza vijana na kinababa kujitokeza kwa wingi kupaga kura na kumchagua mgombea anayetokana na CCM.

Mwisho...

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS