Header Ads Widget

DUWASA YAJIPANUA MAENEO YA PEMBEZONI.


Na Hamida Ramadhani, Matukio Daima App, Dodoma.

MAMLAKA ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imejipanua zaidi na Sasa wanahudumia Wilaya za pembezoni Kama vile Chamwino,Gongwa ,Kibaigwa na Bahi ambapo kwa Kanda ya Chamwino Mamlaka hiyo inainahudumia wakazi wapatao 44,269 ikiwa na idadi ya wateja 3,020. 


Hayo yamesemwa leo Jijini hapa na Mkurungezi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Mhandisi Aron Joseph Wakati akitoantaarifa kwabwaandishi was habari kuhusu utendaji was majukumu yake na muelekeo was bajeti kwa Mwaka was Fedha 2023/24  


Amesema Eneo la huduma kwa mji wa Chamwino ni vijiji vitano yaani Chamwino, Buigiri, Msanga, Chinangali II na Mwegamile. 


Amesema Hali ya upatikanaji wa Maji imeboreshwa kutoka asilimia 61% hadi 89% mradi wa miji 28 unategemea kuboresha Zaidi huduma ya upatikanaji maji safi kufikia asilimia 95% kazi ya usanifu inaendelea. 


Ameeleza kuwa ,Uzalishaji wa MajiMahitaji ya sasa ya maji kwa maeneo haya ya kata tatu za Buigiri, Msanga na Chamwino ni wastani wa meta za ujazo 4,500 kwa siku (4,500m3/day) Kiasi kinachozalishwa ni mita za ujazo 4580 kwa siku kwa masaa 20 (4,580m3/day). 


Msikilize hapa Mkurungezi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA):



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI