Na Gift Mongi MATUKIO DAIMA APP,Moshi.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi(UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirima amesema julai 15 mwaka huu kutafanyika kikao cha kikatiba cha baraza la umoja huo na kuwa maandalizi yote yapo tayari.
'Niseme tu jambo linaendelea Moshi Vijijini hakuna kupoa siku zinahesabika hivi sasa na wajumbe wake mkao tayari kwa tukio hili'imeeleza taarifa hiyo aliyoitoa kwa waandishi wa habari
Aidha amesema kuwa maandalizi yote muhimu tayari yameshakamilika ikiwa ni pamoja na eneo la kufanya kikao hicho ambapo ni katika ukumbi wa mikutano wa chama wilaya lakini pia kutaarifu wajumbe kama taratibu zinavyoelekeza
0 Comments