NA MBARUKU YUSUPH,Matukio Daima APP Tanga
WIZARA ya Elimu ,Sayansi na Technolojia imeanza kutekeleza ahadi ya Rais kwa Watanzania juu ya mageuzi ya elimu inayotolewa sasa na kwenda kwenye mfumo wa elimu ya mafunzo ya amali yatakayomuwezesha mwanafunzi kujiajiri au kuajiriwa baada ya kuhitimu.
Hayo yamebaishwa na Waziri wa Wizara hiyo Prof, Adolf Mkenda wakati wa Ziara yake ya Siku mbili Mkoani hapa iliyokuwa na lengo la kutembelea kituo cha kisayansi cha Stem park ,Veta na Shule ya Sekondari ya Tanga Tech ambayo inatoa mafunzo ya amali ya uhandisi na shule hiyo ndio iliyochaguliwa kuanza kutumika kwa mafunzo ya amali kuanzia january mwakani.
Alisema mageuzi ya elimu yanayotakiwa kufanywa na Serikali na kwenye moyo wa mageuzi hayo kuna mafunzo ya amali ambayo ndio mafunzo ya kazi kwa kiswahili sanifu ni istilahi neno ambalo linatumika sana kwa wenzetu wa Zanzibar.
Prof,Mkenda alisema Rais alitoa ahadi hiyo kwa Watanzania kwamba kutafanyika mageuzi ya elimu ambayo yatawaandaa vijana kwenda kujishughulisha na kazi au kuajiriwa huku wakiwa wameshaandaliwa badala ya kusubiri wamalize na kuhitimu na kushindwa kuajiriwa.
Aidha Prof,Mkenda alisema tayari rasimu ya mapitio ya sera ya elimu ya 2014 toleo la 2023 imekamilika na kiufasaha itajulika kama 'sera ya elimu na mafunzo ya 2014 toleo la 2023"
"Kwa sababu hatuna mambo mengi ya kubadilisha na kama kweli tunahitaji kuwa na Wizara iliyotulia na si Wizara ambayo kila anayekuja anaanzisha jambo lake lazima tujidhatiti kwa mageuzi haya ya elimu "Alisema Prof Mkenda.
Alisema sera hiyo iliasisiwa na Dkt Kawambwa wakati wa Rais wa awamu ya nne na baada yakuipitia sera hiyo sambamba na kukaa na wadau mbalimbali wa elimu waligundua mambo mengi ndani ya sera hiyo hayakutekelezwa jambo lililopelekea Wizara hiyo ya Elimu ichukue hatua ya kutekeleza Mapendekezo ya sera hiyo.
"Bahati nzuri tumeshamaliza mchakato wote na kilichobakia ni kupeleka mageuzi hayo katika baraza la Mawaziri ingawa jambo hili litachukua muda lakini tutawahitaji Mawaziri wenzetu watuunge mkono katika jambo hili" Alisema.
Mbali na hayo pia Prof Mkenda alipata fursa ya kutembeleakituo cha Sayansi cha Stem Park kinachomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Tanga ambacho kipo kwa ajili ya kuendeleza masomo ya Sayansi,technolojia na ubunifu kwa njia ya vitendo kwa wanafunzi.
"Wenzetu wa Project Inspire waliniomba nije katika kituo hiki cha Stem Park ili niangalie wanachofanya na wanataka kusain MOU na Wizara yetu kwa ajili ya ushirikiano na nimepata fursa ya kuja kuangalia nimeona wanavyofundisha Sayansi na Technolojia kwa vitu vinavyopatikana hapa Nchini"Alisema.
Mafunzo ya vitendo ya kisayansi yanayofanyika katika kituo hiki yanasaidia sana mtu kuelewa na hii itakuja kusaidia kipindi kinachokuja kwa kuwafundisha watoto kwa njia ya kuwafikirisha ili waweze kufikiria wenyewe na waweze kujitahidi kufanya uvumbuzi mbalimbali.
Alisema kituo hicho kinaonekana kuwa ni kitu muhimu sana kwa ajili ya kuchochea uwelewa wa Vijana na mbali ya Tanga kipo kingine Jijini Dar es Salaam na ni wakati sasa wa kuanzisha kituo kikubwa zaidi Mkoani Dodoma ambapo ndio Makao Makuu ya Nchi.
Prof,Mkenda alisema umuhimu wa kuanzishwa kwa kituo kama hicho Mkoani Dodoma ni kutoa fursa kwa Mawaziri,Wabunge,Wakuu wa Mikoa ,Wakuu wa Wilaya na watu mbalimbali waweze kutembelea kwenye kituo hicho na waone nini kinaweza kufanyika katika maeneo yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Project Inspire Lwidiko Edward alisema kazi ya taasisi hiyo ni kuwalea watoto kutokana na udadisi wao wa ki asili wa Sayansi ili kuwatengeneza kuwa wana Sayansi halisi.
Edward alisema miongoni mwa vitu wanavyopendezewa kuvifanya katika kituo hicho ni pamoja na kutoa mafunzo hayo kwa wanafunzi ambao ni wadogo ili kuwapa hamasa katika masomo ya Sayansi na kumfanya kuwa mtaalamu katika maswala ya Sayansi,Technolojia, uhandisi na Mahesabu.
"Nchi zilizoendela asilimia kubwa ya pato la Nchi linatokana na Taaluma hiyona tunahitaji Tanzania tufukie huko"isema Edward.
0 Comments