Na Fadhili Abdallah,Kigoma
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ametoa maelekezo kutolewa kwa kiasi cha kiasi cha shilingi milioni 300 ajili ya kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika mji wa Kibondo kutokana na deni la bili ya umeme na uwezo mdogo wa matanki ya kuhifadhi maji mambo yanayosababisha kudumaa kwa huduma kwa wananchi.
Waziri Aweso ametoa maelekezo hayo akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Community Centre mjini Kibondo ambapo sambamba na fedha hizo ametoa maelekezo kupatiwa pikipiki nane na gari moja kwa mamlaka ya maji safi na maji taka katika mji wa Kibondo (KIUWASA) kuimarisha utendaji wa mamlaka hiyo.
Waziri Aweso alikuwa akipokea taarifa na salamu za Meneja wa Mamlaka ya maji safi na maji taka Kibondo, Aidan Ngatomela zinayoeleza namna changamoto ya kushindwa kupatikana kwa fedha hizo kunavyokwamisha usambazaji wa maji safi na salama kwenda kwa wananchi wa mji wa Kibondo.
Katika fedha ambazo Waziri Aweso ameagiza kutolewa ni pamoja na shilingi milioni 100 kwa ajili ya kumaliza deni la umeme ambalo mamlaka ya maji ya mji wa Kibondo inadaiwa na TANESCO wilayani humo.
Fedha nyingine ambazo Waziri Aweso ameagiza kutolewa ni kiasi cha shilingi milioni 200 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa tanki la kuhufadhia maji lenye ujazo wa lita milioni 1.5 ambalo limekwama kukamilika kwa sababu fedha hizo hazipatikani kumalizoa kazi hiyo.
Awali Meneja wa Mamlaka ya maji safi na maji taka wilaya Kibondo, Aidan Ngatomela 0alisema kuwa hali ya upatikanaji maji kwa mji wa Kibondo ni asilimia 61 lakini hali hiyo imeshuka hadi asilimia 47 kutokana na changamoto ya deni la TANESCO shilingi milioki 104 ambalo limekuwa taabu kulipika hivyo upatikanaji wa umeme kwa ajili ya kupampu maji kwenda kwa wananchi unakuwa wa shida.
Sambamba na hilo Meneja huyo alisema kuwa wanao ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji kwa ujazo wa lita milioni 1.5 lakini milioni 288 zinahitajika kumalizia ujenzi huo ili tanki hilo liwezeshe usambazaji maji kwa mji wa Kibondo kufikia asilimia 100.
0 Comments