Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Changamoto ya uhaba wa usafiri (ambulance) kwa ajili ya kuwasafirisha wanawake wajawazito kwenda kwenye vituo vya rufaa wanapopata changamoto wakati wa kujifungua ikielezwa kuwa moja ya visababishi vikubwa vya kuendelea kwa vifo vya mama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua mkoani Kigoma.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya la umoja wa Mataifa (WHO), Nemes Iriya alisema hayo wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakati shirika hili lilipokabidhi gari mbili za kubeba wagonjwa wa dharula (Ambulance) zilizotolewa kwa halmashauri za Kigoma na Buhigwe za mkoani Kigoma.
Mwakilishi huyo wa WHO alisema kuwa bado vituo vingi vya kutolea huduma havina vifaa vya kutosha kusaidia kukabilia matatizo ya mama wajwazito wakati wa kujifungua hivyo wanapopata matatizo wanapaswa kukimbizwa kwenye vituo vikubwa vya afya au hospitali ili kupata usaidizi wa kitaalam lakini bado hakuna gari za kutosha za kubeba wagonjwa kuwezesha jambo hilo kufanyika kwa haraka.
Alisema kuwa Tanzania imepiga hatua katika kukabiliana na vifo vya mama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua lakini bado jitihada zaidi zinapaswa kufanywa kwa wadau wote kuunganisha nguvu kwa pamoja na hasa katika kutekeleza mpango mkakati wa serikali wa mwaka 2021 hadi 2025 ambao unazungumzia pia kukabiliana na vifo vya mama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua.
Awali Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA), Mark Schreiner akizungumza kabla kukabidhi jengo la kujifungulia kina mama kwenye zahanati ya Kigondo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma alisema kuwa Ulimwengu alisema kuwa vifo vya mama wajawazito na watoto bado changamoto kubwa mkoani Kigoma na jitihda zinapaswa kufanywa kukabiliana na hali hiyo.
Akitoa takwimu za hali ya vifo hivyo alisema kuwa kwa mwaka jana mama wajawazito 102 walifariki huku takwimu zikionyesha kuwa kwa mwezi januari pekee ambapo kwa mwaka huu mama wajawazito 26 walifariki na kwamba jambo hilo halikubali kuona mwanamke hata mmoja akifariki wakati wa kujifungua.
Wakizungumza wakati wa makabidhiano hayo baadhi ya wananchi wa kjiji cha Kigondo akiwemo Anastazia Bilamuka alisema kuwa changamoto kubwa inaanza wamama wanapoumwa na uchungu wakiwa nyumbani hakuna usafiri wa uhakika kuwawahisha kwenye vituo vya huduma na hata wanapofika vituoni wanapokosa huduma hakuna gari za kuwapeleka kwenye vituo vya afya vikubwa.
Mwananchi huyo alisema kuwa gharama kubwa ya usafiri kutoka nyumbani kwenye kwenye zahanati au kutoka zahanati kwenda vituo vya afya na hospitali kubwa imekuwa moja ya sababu ya wanawake wengi vijijini kujifungulia nyumbani.
0 Comments