Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan amewahakikishia watanzania kwenda kuanza utekelezaji wa miradi mikubwa ya liganga na mchuchuma wilayani Ludewa mkoani Njombe baada ya kuanza ulipaji fidia kwa wananchi.
Akizungumza kwa njia ya simu na mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka wakati wa uzinduzi wa zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha maeneo yenye madini hayo Rais Samia amesema ni lazima wananchi wote walipwe fidia pamoja na kushughulikia changamoto zote ili miradi hiyo mikubwa ianze.
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la maendeleo la taifa NDC Dkt Nicolaus Shombe amesema Hadi Jana usiku Watu 39 walikuwa wameshalipwa fedha zao za fidia waliopisha maeneo ya uwekezaji wa madini ya Chuma na Makaa ya mawe Wilayani Ludewa mkoani Njombe na zoezi linaendelea.
Mbunge wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga anasema licha ya wananchi wake kuanza kulipwa fidia Lakini bado wanatamani kusikia miradi ya madini hayo inaanza lini kwani wawekezaji wadogo wa mkoa wa Njombe nao wanataka vitalu vya madini.
Waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Dokta Ashatu Kijaji wakati akizindua zoezi la ulipaji fidia wananchi wilayani Ludewa amesema wizara sasa inaanza kwa kasi kubwa kutekeleza mradi wa madini hayo baada ya Serikali kuwalipa wananchi fedha zao.
Face Mhagama na Otmary Witulo ni baadhi ya wananchi waliolipwa fidia ambao wamekiri kupokea fedha hizo na kwamba wanakwenda kuwekeza katika shughuli za maendeleo.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema hakuna ubabaishaji uliotokea wakati wa mchakato wote wa ulipaji fidia hizo.
0 Comments