WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ametoa muda wa miezi mitatu Kwa mkandarasi anayejenga mradi wa Maji wa Uwambingeto Jimbo la Kilolo kukamilisha mradi huo.
Waziri Aweso ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji Cha Uwambingeto Jimbo la Kilolo mkoani Iringa .
Alisema kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi Kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maji ukiwemo mradi huo wa Uwambingeto hivyo Lengo la Rais kuona anamtua mama ndoo kichwani Kwa kumaliza kero ya Maji .
Hivyo alisema Kwa kuwa mradi huo ulilenga kutatua kero ya Maji Kwa wananchi anataka Lengo hilo litimie kama ilivyokusudiwa na si vinginevyo .
Waziri Aweso alisema kuwa hakutakuwa na muda wa kuongeza Katika Utekelezaji wa mradi huo na kuwa ndani ya miezi mitatu kuanzia leo mradi huo uwe umemamilika na unatoa Maji .
Awali mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Dr Rita Kabati na mbunge wa Jimbo la Kilolo Justin Nyamoga walipongeza maagizo hayo ya Waziri Aweso kuwa yataleta ukombozi Kwa wananchi .
Pia wabunge hao wamempongeza katibu mkuu wa CCM Daniel Chongolo Kwa kutoa agizo Kwa Waziri wa Maji kufika kijijini hapo .
Aweso amefika kijijini hapo ikiwa ni siku ya pili toka katibu mkuu wa CCM Daniel Chongolo kutoa muda wa siku 10 Kwa Waziri Aweso kufika kijijini hapo kutatua kero ya Maji .
0 Comments