Na HADIJA OMARY,MATUKIO DAIMAAPP
LINDI…..Wazazi na walezi mkoani Lindi wametakiwa kuwa makini na matumizi ya teknolojia bila kuathiri usalama na makuzi ya watoto kwa kutumia (TEHAMA) wakiaswa kurejea kwenye malezi bora kwa kuwafunza maadili mema.
Wito huo umetolewa na Mkaguzi msaidizi wilaya ya Lindi, Thadei Minja jana wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika kata ya Mnazi mmoja Manispaa ya Lindi , Mkoani humo.
Maadhimisho hayo yaliandaliwa na watoa huduma ya mtoto Klasta ya Lindi waliochini ya Makanisa ya Anglican , Biblia , P.A.G na T.A.G kwa ushirika wenza na Compassion Tanzania Mkoa wa Lindi.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Lindi Thadei Minja alimesema licha ya uwepo wa sanyansi na teknolojia kuchangia kwa kiwango kikubwa maendeleo lakini zipo athari za malezi na makuzi ya watoto, Ndani ya jamii .
Alisema kwa sasa vifaa vya Kielekroniki vikiwemo simu za mkononi vinachukua muda mwingi wa watoto na hata kuwaathiri kisaikolojia na kwamba ili kukabiliana na athari hizo ni wakati muafaka kwa wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao kwa kuhakikisha wanaweka mfumo bora ili kuwalinda na athari zinazoweza kutokea.
“ Kwenye ulimwengu wa kidigitali je Watoto wetu tunawalinda? Atuwapi simu zetu wacheze michezo ya kwenye simu (game) ? Nyie mnawaachia mnaona kama vile mnawapenda lakini mnawaaribu. Kumbuka simu yako inavitu vyako vya kiutu uzima, ukimpa acheze michezo ya kwenye simu (game) watoto wa siku hizi ni wajanja sana atatoka kwenye hiyo michezo akishalichoka atatafuta mchezo mwingine anaingia kwenye Instagram akiona vile vitu hataenda kujaribu huko nje?”Alifafanua Minja .
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mnazi Moja Said Mchinjita alisema ili siku hiyo ya mtoto wa Afrika iweze kuleta tija kwa jamii ni muhimu wazazi na walezi, kuendelea kuwekeza katika elimu ikiwa sambamba na kufuatilia maendeleo ya Mtoto huyo.
Aidha Mchinjita alisema swala la wazazi na walezi kuwaachia simu Watoto wao limekuwa kama fasheni, jambo ambalo sio zuri kwa ulinzi wa mtoto. Hivyo wazazi wanapaswa kuwa na mipaka ya uhuru wa Watoto wao.
Nae mjumbe wa kamati ya huduma ya Malezi alisema kupitia vituo vyao vitano vilivyopo Mkoani Lindi, ambayo vinahudumia Watoto kuanzia miaka mitatu wamekuwa wakitoa Elimu mbali mbali zinazowahusu Watoto wenyewe pamoja na usalama na haki zao za msingi kama elimu na huduma za Afya.
Nae Mwalimu kutoka kituo cha huduma P.A.G Lindi Lowassa Molel alisema, Moja ya vitu wanavvyowafundisha Watoto walionao katika vituo hivyo ni maswala ya ukatili wa kijinsia ambapo zipo kauli mbiu mbali mbali wanazotumia ili kuwakumbusha Watoto.
“Mfano tunawaambia siri yangu usimruhusu mtu kushika, iwe mbele iwe nyuma ,usimruhusu mtu kushika siri yako. tunawaambia na hata wakipita mtaani ni hivyo hivyo”.
Kwa upande wake Mariamu Nanguka Mkazi wa Kata hiyo ya Mnazi mmoja alisema kuwa bado Elimu inahitajika kwa Wazazi na Walezi juu faida na athari za matumizi ya Tehama na teknolojia kwa Watoto wao.
Kwa mujibu wa Taarifa ya hali ya ukatili wa watoto Mtandaoni (Disrupting Harm Report in Tanzania – 2021) inaonesha kuwa katika kila nchi Duniani Watoto ndilo kundi linaloongoza kwa utumiaji wa bidha za mawasiliano zikiwemo simu janja, kompyuta na intaneti kwa ujumla, ambapo nchini Tanzania asilimia 67 ya watoto wenye umri wa miaka 12 – 17 hutumia mitandao ikiwemo simu na intaneti.
Watoto hao hutumia simu za ndugu zao wa karibu wakiwemo Wazazi, Walezi, marafiki na ndugu wengine wanaowazunguka. Pia, taarifa hiyo inaeleza kuwa asilimia 4 ya watoto ni wahanga wa aina mojawapo ya ukatili wa mtandaoni ikiwemo kulazimishwa kujihusisha na vitendo vya kingono, kusambazwa picha na video zenye maudhui ya kingono bila ridhaa yao. Aidha, hurubuniwa kujihusisha na shughuli za kingono kwa kuahidiwa fedha au zawadi zingine
Tarehe 16 Juni, ya kila mwaka, nchi wanachama wa Umoja wa Afrika ikiwemo Tanzania huadhimisha siku ya mtoto wa Afrika ambapo chimbuko la maadhimisho haya ni mauaji ya watoto takribani 2,000 yaliyofanywa na Utawala wa Makaburu katika Kitongoji cha Soweto, nchini Afrika Kusini tarehe 16 Juni, 1976.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mwaka 2023 ni “Zingatia usalama wa mtoto katika ulimwengu wa kidijitali”
MWISHOOO
0 Comments