CHAMA Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Mkoa wa Pwani kimepokea shilingi milioni 28 kwa ajili ya kutoa elimu kwa Watendaji na Wenyeviti waweze kuwashirikisha kundi hilo kwenye kamati mbalimbali ikiwemo ya afya.
Hayo yamebainishwa na mjumbe wa Chama hicho Tatu Kondo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari muda mfupi baada ya kufunguliwa kwa semina ambayo inafanyika kwa ufadhili wa Shirika la Foundation For Civil Society.
Kondo amesema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kutoa elimu ya ujumuishwaji kwa watu wenye ulemavu katika vyombo vya watoa maaamuzi.
Amesema elimu hiyo itatolewa kwa kata sita za mradi ikiwemo Mailimoja, Mlandizi, Kongowe, Mtambani, Visiga na Kilangalanga.
Akifungua semina hiyo ya siku mbili iliyofanyika mjini Kibaha ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Grace Tete amesema viongozi wanatakiwa kuwatambua watu wenye ulemavu kwenye maeneo yao.
Tete amesema viongozi wanatakiwa kuwa na takwimu za watu wenye Ulemavu ili miradi ikiibuliwa iwaguse watu wa makundi yote..
Aidha ameelekeza kuw kamati zinazoundwa watu wenye Ulemavu washirikishwe ili wapate wawakilishi wa kuwasilisha mahitaji yao yapatiwe ufumbuzi.
0 Comments