Header Ads Widget

WANANCHI WA KIJIJI CHA MAGOYE MAKETE NJOMBE WATISHIA KUSUSIA SHUGHULI ZA MAENDELEO BAADA YA MWENYEKITI WAO KUSIMAMISHWA KAZI

 







Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Baada ya  kusimamishwa kazi  mwenyekiti wa kijiji cha Magoye kata ya Itundu wilaya ya Makete mkoani Njombe  bwana Shadrack Malila kwa miezi saba sasa,wananchi  wametishia kugomea kushiriki shughuli za maendeleo Kwa Lengo La Kuushinikiza Uongozi Ngazi Ya Kata Na Wilaya Kumrudisha Mwenyekiti Wao Mamlakani.


Msimamo wa wananchi wa kijiji cha Magoye kutishia kutoshiriki utekelezaji wa miradi ya maendeleo umetolewa katika mkutano wa hadhara kijijini hapo kwa lengo la kufikisha kilio chao kwa viongozi wa ngazi ya kata ya Itundu na wilaya ya Makete.


Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho akiwemo  Lazaro Kyando,Fadili Sanga Na  Tumpe Mbara wanasema hawapo tayari kushiriki shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa ofisi ya kijiji mpaka pale mwenyekiti wao aliyesimamishwa kazi na viongozi wa CCM atakaporejeshwa madarakani.


Kwa upande wake mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho Bwana Shadrack Malila ambaye amesimamishwa Na uongozi wa chama cha Mapinduzi ngazi ya kata ya Itundu na Serikali,amesema anashangazwa na hatua iliyochukuliwa dhidi yake.


Kutokana na sakata hilo kituo hiki kimeongea na  katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Makete Bwana Daniel Mhanza na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Makete Bwana William Makufwe kwa njia ya simu kwa lengo la kujua suluhisho la malalamiko ya wananchi hao.


Subira ndiyo suala pekee linalohitajika katika kipindi hiki kwa wakazi wa Magoye ili waweze kupata suluhu hapo june 29 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI